HABARI MPYA LEO  

Mahalu ashinda kesi

By Mhariri - Aug 10, 2012

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewasafisha aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2 Milioni.

Kutokana na uamuzi huo, Profesa Mahalu amesema anamshukuru Mungu akisema, yaliyotokana ni kwa sababu Mungu amempenda. “Mungu amenipigania sana na haki imetendeka, sasa hivi nakwenda kanisani kumshukuru Mungu, nanyi nawaambieni mkasome Zaburi 17,” alisema Profesa Mahalu kwa furaha na kukumbatiana na mawakili na ndugu zake.

Profesa Mahalu na Martin walikuwa wakikabiliwa na mashtaka sita yakiwamo ya kula njama na kuiibia Serikali na kuisababishia hasara ya Euro 2,065,827.60, katika mchakato wa ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

Hata hivyo,  jana Mahakama hiyo iliwaachia huru ikisema kuwa upande wa mashtaka katika kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2007, umeshindwa kuthibitisha mashtaka hayo bila kuacha mashaka.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII