Tuzo ya CECAFA yazua mzozo.
By Mhariri - Dec 10, 2012
Mshambulizi wa timu ta taifa ya soka ya Uganda
Cranes, Uganda, Robert Ssentongo, ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa
mashindano ya CECAFA Tusker Senior Challenge Cup, yaliyomalizika mjini
Kampala.
Sentongo hata hivyo alifunga magoli manne pekee wakati wa mashindano hayo.
Wachezaji waliofunga idadi magoli mengi kuliko Sentongo,Mrisho Ngassa na John Bocco wa timu ya Tanzania bara, walinyimwa tuzo hilo, na kamati ya ufundi ya mashindano hayo.
Katika mashindano yaliyopita, mchezaji aliyefunga idadi kubwa ya magoli ndiye huibuka mshindi wa taji hilo, lakini mwaka huu mambo nchini Uganda yalikuwa tofauti.
''Ngassa
na Bocco walifunga magoli matano kila mmoja na ilitarajiwa wangepewa
tuzo ya mfungaji bora lakini katika hali ya kushangaza kamati ya CECAFA,
ilimpa tuzo hilo mshambuliaji wa Uganda, Robert Ssentongo aliyefunga
magoli manne'' Alisema kocha wa Kilimanjaro Stars.
Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi wa
mechi ya fainali kati ya Uganda Cranes na Kenya, Ghiery Nkurunziza
kutoka Burundi, Sentongo ndiye aliyefunga bao la ushindi la Uganda,
lakini kuna habari za kutatanisha kuwa, bao hilo lilikuwa la kujifunga.
Hata hivyo, ushahidi wa picha za televisheni
unaonyesha kwamba beki wa Kenya, Anthony Kimani, alijifunga magoli yote
mawili ya fainali.
Baada ya mechi hiyo ya fainali, kipa wa Harambee
Stars Duncan Ochieng anaripotiwa kughadhabishwa sana na kitendo hicho
cha Kimani kiasi cha kutaka kupigana na beki huyo, kwa kusababisha Kenya
kupoteza Kombe hilo.
Wengine waliotuzwa baada ya mashindano hayo ni
pamoja na Brian Umony, ambaye alitangazwa kuwa mchezaji bora, Hamza
Muwonge kutoka Uganda naye aliibuka Kipa bora baada ya kufunga bao moja
pekee wakati wa mashindano hayo.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII