ICC kutoa hukumu dhidi ya Lubanga leo
By Maganga Media - Mar 14, 2012
Bw Lubanga anatuhumiwa kuongoza wapiganaji wa kabila la Wahema katika makabiliano ya wenzao Walendu katika vita vilivyotokea miaka kumi iliopita katika mkoa wa Ituri.
Muasi huyo amekanusha mashtaka yanayomakabili na anasisitiza kuwa yeye alikuwa mwanasiasa na sio mpiganaji.
Makundi yakutetea haki za binadamu yanasema utafiti wao umeonyesha kuwa zaidi ya watu elfu 60 waliuawa katika vita hivyo katika eneo la Ituri ambapo Thomas Lubanga alikuwa na ngome yake.
"Utafiti wetu unaonyesha kuwa uhalifu wa kivita ulitendeka, wanawake walibakwa, watu waliteswa na wengine walizuiliwa bila kufanya makosa yoyote wakati wa vita hivyo vya kikabila. Ni matumaini yetu kuwa hukumu ya leo itakuwa ishara kuwa haki itatendeka" alisema Bi Anneke Van Woudenberg wa shirika la Human Rights Watch.
Thomas Lubanga ndio kiongozi aliyefunguliwa mashataka lakini mwenzake Jenerali Bosco Ntaganda bado hajachukuliwa hatua zozote na anatumikia jeshi la DR Congo.
Kesi hii imedumu kwa muda mrefu na hukumu hii inasubiriwa kwa hamu ni wakaazi wa Ituri ambao bado wanamakovu ya vita hivyo.
http://maganga-resources.blogspot.com
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII