HABARI MPYA LEO  

Mafreemason watinga Clouds FM

By Maganga Media - Jun 8, 2012


 Pichani ni Dkt. Kemu Mzee (kushoto) na Alhaj Prof. Dkt. Salim Kungulila (kulia) wanaojiita Freemasons walio temebele kituo cha Clouds FM leo asubuhi kwenye kipindi cha Leo tena na kuelezea ufreemason wao


Hapa Alhaj Prof. Dkt. Salim Kungulila kutokea Magomeni Mikumi Dsm. Ni mwalimu wa dini mbali mbali. Pichani akielezea ancho jua kuhusu ufreemason na namba 666 ambapo alishindwa kukiri ufreemason wake bali alismea yeye ni MuaashiHuru


 Hahaha huyu ndiye Dkt. Kemu Mzee ambaye yeye alijieleza akasema ni mganga wa tiba asilia na ni Freemason wa Kisukuma.

---


Wanadai wao wanafundisha dini zote na kudai kua kila mtu duniani ni Freemason na pia wafafanua maana halisi ya ufreemasons ila mwisho wasiku walishindwa kujibu kama wao ni mafreemasons au laaah! Wakaishia kusema wao ni WaashiHuru…



 Walipo ulizwa kama freemason wanaabudu shetani wakashindwa kujibu.



Dkt. Kemu Mzee alisema ufreemason ni kitu ambacho hukioni na ni kama kuuza bidahaa haraka haraka kabla ya mwenzio so hapo wewe uliye uza haraka haraka ndo unatajirika haraka.



Walipo ulizwa juu ya masharti ya kujiunga waksema yanapatikana ofisini kwao na ni lazima mtu apate matibabu yao ambayo ni lazima na kuongezea ni sawa na kujiunga na chama fulani ukafuata masharti yao so kwa upande wao tiba yao ndo lazima.



Na Alhaj Prof. Dkt. Salim  alisema watu wanapo ambiwa majini wanaogopa lakini watu wasihofu maana majini ni kama mashine. Mpaka sasa sielewi alimaanisha nini  hahaha!!! 



Kwa kumalizia waliulizwa kama freemason wanatakiwa kutoa sacrifice (kafara) ya ndugu wa karibu wakasema sacrifice (kafara) kila mtu anatoa wakristo au waislamu. Hiyo yakutoa watu ni uzushi pengine.



Hahaha hakuna siku nimecheka kama leo maana hawa jamaa nahisi walienda kuuza sura walikuwa wanapiga chenga maswali na kujibu yao tu.



Kwa hiyo kuconclude na kutokana na maelezo yao wao wamejiita WAASHIHURU tafsiri yake FREEMASON!

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII