Walioleta zengwe Halmashauri ya Tarime kukatwa mshahara
By Maganga Media - Jun 8, 2012
Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za mitaa (LAAC) imeagiza watendaji wakuu wa halmashauri ya Tarime mkoani Mara kukatwa asilimia 15 ya mshahara wao wa mwezi june kama adhabu kutokana na uzembe uliofanywa katika kuandaa hesabu za Halmashauri hiyo.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Idd Azan amesema watakaokatwa mishahara yao ni Mkurugenzi wa halmashauri Fideris Lumato, mtunza hazina wa Halmashauri Joash Maganga na mkaguzi wa ndani wa halmashauri Elias Amede huku watendaji wengine wakitakiwa kuandikiwa barua ya onyo.
Katika kikao kati ya kamati hiyo na uongozi wa halmashauri hiyo ya Tarime, Azan amesema hesabu zilizowasilishwa kwenye kamati haziridhishi hivyo kuagiza ukaguzi maalum ufanyike ndani ya mwezi mmoja katika baadhi ya miradi ikiwemo ya barabara na kama kutakua na jinai hatua zichukuliwe.
Kuhusu kuwepo kwa stori za wajumbe wa LAAC kuhojiwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Makamu Mwenyekiti huyo amesema hana taarifa za wajumbe wa kamati yake kuhojiwa na kama anahojiwa mmoja mmoja basi kila mtu atasema lakini kuna uwezekano ikawa anahojiwa mtu mmoja mmoja.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII