Kenya yaomba msaada EU kupambana na Al-shabab!
By Maganga Media - Jun 13, 2012
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ameomba msaada kifedha na vikosi kutoka Marekani na Ulaya kuwatoa al-Shabab kwa ‘shambulio la mwisho’ katika mji wenye bandari wa Kismayo.
Raila Odinga alisema vikosi vyaKenya vinatarajia kuingia Kismayo mwezi Agosti na alisema al-Shabab itahitaji "operesheni ya kivita ardhini, baharini na angani".
Lakini msemaji wa sera za nje wa Muungano wa Ulaya Michael Mann alisema hiyo ni kwenda kinyume na majukumu yake.
Manowari za kivita zimekuwa katika eneo hilo tangu mwaka 2008 kupambana na maharamia. Majukumu yake hivi karibuni yaliongezeka ili kuruhusu mashambulizi ya ardhini dhidi maharamia wa Kisomali. Hadi manowari kumi za kivita zinafanya doria katika Pembe ya Afrika kama sehemu ya harakati ya Muungano wa Ulaya ‘Atalanta’ ambayo ilianzishwa kulinda biashara za bandarini dhidi ya mashambulizi ya maharamia.
Bw Mann alisema: "Hatuna budi kuwa makini sana kufanya harakati zetu katika mzingo wa sheria za kimataifa. Tunawajibika katika jukumu letu ambalo ni kupambana na maharamia baharini kwa kuharibu mgome zao.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII