HABARI MPYA LEO  

Mkuu wa pilisi Afrika Kusini afutwa kazi

By Maganga Media - Jun 13, 2012


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amemfuta kazi mkuu wa polisi Generali Bheki Cele, aliyekuwa ametuhumiwa kwa makosa ya rushwa.Bwana Zuma aliambia waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake na pia kuhusu atakayechukua nafasi yake akiwa ni bwana Mangwashi Phiyega. 

Hatua hii inamfanya bi Mangwashi kuwa mkuu wa kwanza wa polisi mwanamke.

Generali Cele, ambaye mtangulizi wake alifungwa jela kwa tuhuma za ufisadi, alihukumiwa mwezi Oktoba baada ya taarifa kuhusu kuhusika kwake katika kashfa uuzaji haramu wa nyumba za polisi ingawa alikanusha madai hayo.Inaaminika alihusika na kampeini ya rais Zuma wakati wa kampeini za uchaguzi wa rais mwaka 2009.

Mwaka jana afisa anayechunguza kesi za ufisadi ,Thuli Mandonsela, alisema kuwa nyumba za polisi zilikodiwa kutoka kwa kampuni moja ambayo ilipandisha bei ya kukodi na kwamba Cele ndiye alihusika na kashfa ya kupandisha bei ya nyumba hizo. Bi Madonsela ambaye ni mratibu wa malalamiko ya umma alimshtumu Generali Cele kuwa mmoja wa wale waliohusika na kashfa hiyo.

Alichunguza utaratibu wa kukodisha nyumba ambazo zilikuwa za polisi mjini Pretoria na mji wa Mashariki wa Durban na kupata kweli zilipandishwa bei kinyume na sheria. Serikali ya Afrika Kusini imekumbwa na kashfa nyingi za ufisadi katika siku za hivi karibuni.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII