HABARI MPYA LEO  

Bolt aweka historia London

By Mhariri - Aug 10, 2012

Usain Bolt usiku wa Alhamisi alifanikiwa kuwa mwanariadha wa kwanza katika historia ya michezo ya Olimpiki, kuweza kuutetea ubingwa wake kikamilifu katika mbio zote fupi, mita 100 na vile mia 200. Bolt aliwaongoza wanariadha wenzake kutoka Jamaica katika kunyakuwa medali zote tatu katika mashindano hayo ya mita 200.

Muda wa Bolt katika mashindano hayo ulikuwa ni sawa na ule wa Michael Johnson katika mashindano ya Atlanta, na uliokuwa muda bora zaidi wa dunia wakati huo, wa sekunde 19.32. Mwanariadha ambaye hufanya mazoezi na Bolt, Yohan Blake, alipata medali ya fedha, huku Warren Weir akichukua ya shaba. 

Blake alikuwa amemshinda Bolt katika mashindano ya Jamaica ya kufuzu kushirikishwa katika mbio za London, lakini Blake hakuwezana na kasi ya Bolt wakati huu."Hili ndilo jambo ambalo nililitaka, na nimefanikiwa kulipata. Ni fahari kuu kwangu,"

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII