Matokeo ya uchaguzi yahairishwa Misri
By Unknown - Jun 21, 2012
Wagombea hao Mohammed Mursi na Ahmed Shafiq wote wamedai kushinda uchaguzi huo. Kulingana na tume ya uchaguzi jumla ya malalamiko 400 yamewasilishwa lakini haijasema matokeo hayo yatatangazwa lini.
Msemaji wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, Nader Omran amesema kuwa tangazo hilo halifai kuhairishwa. "Hatua hii itachochea hali ya wasiwasi itakuwa bora zaidi suala hili limalizwe alhamisi" amesema Bw Omran.
Wasimamizi wa kampeni ya mgombea wa Muslim Brotherhood, Mohammed Mursi wanasema kuwa kura zinaonyesha kuwa alishinda duru hiyo ya pili ya uchaguzi.
Lakini mshauri wa karibu wa Ahmed Shafiq, amewaelezea waandishi wa habari mjini Cairo kuwa, Shafiq- aliyekuwa waziri mkuu chini ya Utawala wa rais Hosni Mubarak-alishinda uchaguzi huo. Maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani ya Tahriri tangu juzi kulaani baraza kuu la jeshi ambalo juzi limejilimbikizia mamlaka baada ya mahakama kuu kulivunja bunge la nchi hiyo.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII