HABARI MPYA LEO  

Papa ataka amani Nigeria

By Emmanuel Maganga - Jun 21, 2012

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametoa wito wa kokomeshwa kwa kile alichokitaja kama mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wakrito nchini Nigeria. Kiongozi huyo alikuwa akizungumza mjini Vatican wakati wa hotuba yake ya kila wiki.

Siku ya jumapili makanisa matatu yalishambuliwa na watu wa kujitolea mhanga na kusababisha vifo vya watu 16. Wanaharakati wa Boko Haram walidai kuhusika na shambulizi hilo. Kutokana na shambulizi hilo la jumapili ,kumekuwa na mashambulizi mwengine ya ulipizaji kisasi katika miji ya Kaduna na Damaturu na kusababisha vifo zaidi.

Lakini katika hutuba yake Papa Benedict amewataka wa-Nigeria wajenge jamii iliyona maelewano. Amsema amekuwa akifuatilia kwa masikitiko makubwa yale yanayotokea nchini Nigeria ambapo mashambulizi ya kigaidi yanaendelea hasa yakielekezwa kwa wa-kristo. Papa ametaka hali hiyikomeshwe ili kuzuia umwagikaji zaidi wa damu nchini humo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII