Chama cha National Forces Alliance kimeshinda Libya
By Unknown - Jul 18, 2012
Chama cha National Forces Alliance, kinachoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa mpito Mahmoud Jibril kilipata ushindi kwa kunyakua viti 39.
Chama cha mwelekeo wa Dini ya kiislamu cha Muslim Brotherhood kilichukua nafasi ya pili kwa kushinda viti 17.
Bunge hilo la wanachama 200 litakuwa na wabunge wengi wa kujitegemea.
Bunge hilo litakuwa na mamlaka makubwa ambapo linatarajiwa kuunda Serikali mpya ya mpito na wakati huohuo kusimamia shughuli za kutunga Katiba mpya.
Wabunge hao wanapaswa kushikilia madaraka yao kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Nao Raia wa libya wana matumaini kuwa uchaguzi huo ni mwanzo mpya wa utaratibu wa utawala wa kidemokrasia nchini.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII