HABARI MPYA LEO  

Taswira ya Reli ya kati kutoka Dodoma hadi Kigoma

By Mhariri - Sep 9, 2012

TASWIRA YA RELI YA KATI KUTOKA DODOMA HADI KIGOMA
Ninamshukuru Mungu kwa uzima tele na kunipa tena fursa ya kuweza kuandika makala hii inayohusu taswira ya reli ya kati kutoka Dodoma hadi Kigoma mwisho wa reli kama wenyewe walivyozoea kusema. Ni matumaini yangu kuwa utaipenda kwani inaonesha uhalisia wa maisha ya kila siku ambayo watanzania wenzetu wanapitia na kuyaishi ndani ya miaka 50 ya uhuru.

Awali ya yote unaweza kujiuliza kwa nini mwandishi ameanzia Dodoma hadi Kigoma na sio Dar es Salaam hadi Kigoma au kwa nini hakugusia matawi ya reli hiyo kutoka Tabora hadi Mwanza au Tabora hadi Mpanda? Je ungependa kujua na huko kukoje? Utaletewa tu, cha muhimu ni kupata taswira hii kuu kwa hisani ya Maganga Media. Kwa maoni au Ushauri, makala na matangazo tuwasiliane kwa anuani hapo juu, pia weka maoni yako baada ya habari hii ili watu mbalimbali waweze kuyaona na kuchangia.

Hivi karibuni Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa H. Mwakyembe alifanya safari ya kushtukia na akasafiri kwa Treni akitokea Dar es Salaam hadi Dodoma. Kuna mengi alijionea na ikawa chachu ya mabadiliko tunayoyategemea katika shirika hili kongwe nchini linalotegemewa sana kwa wasafiri walioko mikoa ya kanda ya magharibi mwa Tanzania yaani Tabora, Kigoma, Katavi, na kwingineko ambapo huona umuhimu wa kupunguza safari yao kwa kupanda treni na hatimaye kuchukua mabasi hadi makwao ambapo tayari anakuwa amepunguza gharama za usafiri. Ni mengi aliyaona waziri lakini isiwe mwisho akaamini kuwa alimaliza yote, kuna mengine mengi huku mwandishi ameshuhudia na kuamua kuyaweka wazi.

Baada ya kusubiri kwa masaa kadhaa ili usafiri wetu wa treni ufike Dodoma, hatimaye saa nne asubuhi treni ikawasili ikiwa imejaza abiria wengi. Behewa zetu zinazoanzia Dodoma zikaunganishwa na safari ikaanza saa tano na nusu asubuhi. 

Angalia siti za kukalia zilivyochoka. Iliwalazimu abiria kutandika khanga, Taulo au vitambaa walivyoona vinaweza kusaidia kupunguza vumbi na hivyo kuwa katika hatari ya kupata mafua.
 
Watu wakiwa wamesimama na wengine wakiwa wamekaa njiani kutokana na kukosa siti.

MSONGAMANO WA WATU NDIO USISEME. KILA MTU ANATAKA KUSAFIRI

Kufika maeneo ya vijiji vya Singida ambapo kunasifiwa kuwa na kuku wengi si ndio mama mmoja akatoa kituko alipopanda ndani ya treni na kitenga cha kuku wapatao 10 na kukifunga juu kama kinavyoonekana pichani bila kuogopa msongamano wa watu waliokuwa wamesimama pia kwa kukosa siti za kukaa.

Ikumbukwe kwamba utaratibu wa tiketi za treni zinatolewa stesheni, lakini kwa bahati mbaya , wote wanaopandia njiani huwa hawapewi siti za kukaa nah ii ni kutokana na treni kuondoka ikiwa imejaa tangu inatoka kituo kikubwa. Sasa hapa nani alaumiwe kwa watu kusimama? Je, wasisafiri hadi itakapotokea behewa liko wazi kitu ambacho ni ndoto kutokea.
Cheki watoto walivyokusanyana katika moja kati ya stesheni za njiani.
 Chumvi ya UVINZA hii, mfuko sh 500/=
 Kazuramimba
 Kazuramimba, MUWA mmoja sh 500/=
Tuwaletee kiwanda cha sukari wanaweza kuzalisha sukari ya kuwatoshereza mkoa wao na mikoa ya jirani.
 Hiyo juu ni KAZURAMIMBA. Bidhaa zake ni kama unavyoziona
 Kituo cha KATOSHO ambapo mizigo yote ya Biashara kama unavyoina pichani hushushwa hapo. Wananchi wanahoji iweje wao wasumbuliwe kulipia mizigo inayozidi kilo 20 huku ni nguo zao na wafanyabiashara waliobeba mahindi, ubuyu, dengu, mchele na bidhaa zingine kutoka huko wasafirishe bure au kwa gharama nafuu kuliko mwenye begi lake anaenda nyumbani au mwanachuo na sub ufa yake au desktop computer? Mulika mwizi hapo.
 KIGOMA stesheni

 Station ya Kigoma hiyoooooooooo, watu wanasubiria kupokea ndugu zao na wengine wanasubiria kupanda treni hiyo kwenda Tabora, Dodoma , Morogoro na Dar es Salaam.

Pichani kwa juu ya ngazi unaweza kuona watu wamekaa kwa wingi. Wale wapo wanahangaikia tiketi za treni hiyo. Kwa mujibu wa maelezo yao ni kuwa zinasumbua kweli. Eti Kigoma mwisho wa reli, kuingia rahisi kutoka kazi, hii ni balaa. Makala ijayo itajaribu kufuatilia upatikanaji wa tiketi katika station hiyo. Hii yote kwa hisani ya Maganga Media.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII