HABARI MPYA LEO  

From NECTA to Private Candidates CSEE & QT 2012

By Mhariri - Aug 24, 2012

 
TANGAZO

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Katibu  Mtendaji,  Baraza  la  Mitihani  la  Tanzania  anapenda kuwatangazia  Watahiniwa  wote  wa  Kujitegemea  wanaotarajia kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) na Kidato cha Nne (CSEE)  mwezi Oktoba,  2012  kwamba  wametumiwa  barua  zao  za  kusajiliwa kupitia  kwa  Wakuu  wa  Vituo  vya  Mitihani  walikojiandikisha kufanyia mitihani yao. Kila mtahiniwa anatakiwa kwenda kwenye kituo atakachofanyia mtihani kupewa barua yake.

Baraza  la  Mitihani  linasisitiza  kuwa  hakuna  Mtahiniwa atakayeruhusiwa  kufanya  mtihani  bila  ya  kuonesha  barua  ya kusajiliwa. Hivyo ni muhimu kila mtahiniwa mtarajiwa kufuatilia barua  yake  mara  moja  na  kujiridhisha  na  usahihi  wa  taarifa  zilizomo.

 
LIMETOLEWA NA:

KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII