HABARI MPYA LEO  

LEMA AVULIWA UBUNGE

By Maganga Media - Apr 5, 2012


Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema avuliwa ubunge na Mahakama kufuatia kilichoelezwa na Mahakama kwamba ni ukiukaji wa taratibu za uchaguzi, ikiwemo matumizi ya Lugha za matusi. 

 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetoa hukumu ya kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katika kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo. Akitangaza hukumu hiyo Jaji Gabriel Rwakibarila ameyakubali madai mawili kati ya manne yaliyofunguliwa dhidi ya Lema na kutoa hukumu juu ya madai walalamikaji hao kwamba Lema alitoa kauli za udhalalishaji, matusi na kashfa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge wa CCM Arusha Mjini, Dk Batilda Burian. Shauri hilo namba 13/2010 


Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII