HABARI MPYA LEO  

HUKUMU YA LEMA LEO

By Maganga Media - Apr 5, 2012

MAMIA ya wakazi wa jiji la Arusha na maeneo ya jirani leo wanatarajia kujitokeza, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katika kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo. Akizungumzia hukumu hiyo jana, Lema alisema: “Nanamuamini Mungu kwa asilimia 100.” 

Jaji Gabriel Rwakibarila anatarajiwa kutoa hukumu juu ya madai walalamikaji hao kwamba Lema alitoa kauli za udhalalishaji, matusi na kashfa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge wa CCM Arusha Mjini, Dk Batilda Burian. Shauri hilo namba 13/2010 ambalo mshtakiwa wa pili ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), upande wa walalamikaji uliita mashahidi 14. Hata hivyo, Dk Burian hakufika. Upande wa utetezi ukiita jumla ya mashahidi wanne.

Walalamikaji katika kesi hiyo, wanawakilishwa na Mawakili Alute Mungwai na Modest Akida, wakati upande wa utetezi unaogozwa na Wakili, Method Kimomogoro anayemwakilisha Lema, huku AG akiwakilishwa na Mawakili Timon Vitalis na Juma Masanja.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 ambao matokeo ya Jimbo la Arusha Mjini yalitangazwa Novemba 2, Lema alipata kura 56,569 huku Dk Burian ambaye hivi sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, akipata kura 37,460. Katika hati yao ya madai, walalamikaji hao wanadai katika mikutano yake ya kampeni alizofanya sehemu mbalimbali, Lema alisema Dk Burian hastahili kuchaguliwa kwa sababu ameolewa Zanzibar, siyo mwaminifu kwa kuzaa nje ya ndoa na wakati wa mchakato wa uchaguzi alikuwa na mimba ya nje ya ndoa na (Edward) Lowassa.
 
Wadai hao pamoja na mashahidi wote 14, waliieleza Mahakama mbele ya Jaji Rwakibarila kuwa Lema pia alitahadharisha wapiga kura kuwa makini na watu wanaofunga vilemba wasije kujikuta wakichagua Al Qaeda.

Walalamikaji hao wanaiomba Mahakama itengue matokeo yaliyompa Lema ushindi na iamuru walipwe gharama za kesi pamoja na malipo mengine itakavyoona inafaa.

Wakili Kimomogoro pamoja na mawakili wa Serikali,  Vitalis na Masanja walipinga madai hayo wakidai ni ya uongo na yaliyotokana na chuki ya mlalamikaji wa kwanza, (Mkanga) aliyepoteza udiwani mwaka 2007 kutokana na kuandamwa na Lema wakati huo mlalamikaji huyo akiwa TLP.

Katika hoja zao za majumuisho, Wakili Kimomogoro na wenzake wa Serikali waliiomba Mahakama kutupilia mbali madai na ushahidi wa walalamikaji na mashahidi kwa sababu walipingana katika mambo ya msingi katika tukio 
SOURCE: MWANANCHI

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII