HABARI MPYA LEO  

TASWIRA YA RELI YA KATI KUTOKA DODOMA HADI KIGOMA
Ninamshukuru Mungu kwa uzima tele na kunipa tena fursa ya kuweza kuandika makala hii inayohusu taswira ya reli ya kati kutoka Dodoma hadi Kigoma mwisho wa reli kama wenyewe walivyozoea kusema. Ni matumaini yangu kuwa utaipenda kwani inaonesha uhalisia wa maisha ya kila siku ambayo watanzania wenzetu wanapitia na kuyaishi ndani ya miaka 50 ya uhuru.

Awali ya yote unaweza kujiuliza kwa nini mwandishi ameanzia Dodoma hadi Kigoma na sio Dar es Salaam hadi Kigoma au kwa nini hakugusia matawi ya reli hiyo kutoka Tabora hadi Mwanza au Tabora hadi Mpanda? Je ungependa kujua na huko kukoje? Utaletewa tu, cha muhimu ni kupata taswira hii kuu kwa hisani ya Maganga Media. Kwa maoni au Ushauri, makala na matangazo tuwasiliane kwa anuani hapo juu, pia weka maoni yako baada ya habari hii ili watu mbalimbali waweze kuyaona na kuchangia.

Hivi karibuni Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa H. Mwakyembe alifanya safari ya kushtukia na akasafiri kwa Treni akitokea Dar es Salaam hadi Dodoma. Kuna mengi alijionea na ikawa chachu ya mabadiliko tunayoyategemea katika shirika hili kongwe nchini linalotegemewa sana kwa wasafiri walioko mikoa ya kanda ya magharibi mwa Tanzania yaani Tabora, Kigoma, Katavi, na kwingineko ambapo huona umuhimu wa kupunguza safari yao kwa kupanda treni na hatimaye kuchukua mabasi hadi makwao ambapo tayari anakuwa amepunguza gharama za usafiri. Ni mengi aliyaona waziri lakini isiwe mwisho akaamini kuwa alimaliza yote, kuna mengine mengi huku mwandishi ameshuhudia na kuamua kuyaweka wazi.

Baada ya kusubiri kwa masaa kadhaa ili usafiri wetu wa treni ufike Dodoma, hatimaye saa nne asubuhi treni ikawasili ikiwa imejaza abiria wengi. Behewa zetu zinazoanzia Dodoma zikaunganishwa na safari ikaanza saa tano na nusu asubuhi. 

Angalia siti za kukalia zilivyochoka. Iliwalazimu abiria kutandika khanga, Taulo au vitambaa walivyoona vinaweza kusaidia kupunguza vumbi na hivyo kuwa katika hatari ya kupata mafua.
 
Watu wakiwa wamesimama na wengine wakiwa wamekaa njiani kutokana na kukosa siti.

MSONGAMANO WA WATU NDIO USISEME. KILA MTU ANATAKA KUSAFIRI

Kufika maeneo ya vijiji vya Singida ambapo kunasifiwa kuwa na kuku wengi si ndio mama mmoja akatoa kituko alipopanda ndani ya treni na kitenga cha kuku wapatao 10 na kukifunga juu kama kinavyoonekana pichani bila kuogopa msongamano wa watu waliokuwa wamesimama pia kwa kukosa siti za kukaa.

Ikumbukwe kwamba utaratibu wa tiketi za treni zinatolewa stesheni, lakini kwa bahati mbaya , wote wanaopandia njiani huwa hawapewi siti za kukaa nah ii ni kutokana na treni kuondoka ikiwa imejaa tangu inatoka kituo kikubwa. Sasa hapa nani alaumiwe kwa watu kusimama? Je, wasisafiri hadi itakapotokea behewa liko wazi kitu ambacho ni ndoto kutokea.
Cheki watoto walivyokusanyana katika moja kati ya stesheni za njiani.
 Chumvi ya UVINZA hii, mfuko sh 500/=
 Kazuramimba
 Kazuramimba, MUWA mmoja sh 500/=
Tuwaletee kiwanda cha sukari wanaweza kuzalisha sukari ya kuwatoshereza mkoa wao na mikoa ya jirani.
 Hiyo juu ni KAZURAMIMBA. Bidhaa zake ni kama unavyoziona
 Kituo cha KATOSHO ambapo mizigo yote ya Biashara kama unavyoina pichani hushushwa hapo. Wananchi wanahoji iweje wao wasumbuliwe kulipia mizigo inayozidi kilo 20 huku ni nguo zao na wafanyabiashara waliobeba mahindi, ubuyu, dengu, mchele na bidhaa zingine kutoka huko wasafirishe bure au kwa gharama nafuu kuliko mwenye begi lake anaenda nyumbani au mwanachuo na sub ufa yake au desktop computer? Mulika mwizi hapo.
 KIGOMA stesheni

 Station ya Kigoma hiyoooooooooo, watu wanasubiria kupokea ndugu zao na wengine wanasubiria kupanda treni hiyo kwenda Tabora, Dodoma , Morogoro na Dar es Salaam.

Pichani kwa juu ya ngazi unaweza kuona watu wamekaa kwa wingi. Wale wapo wanahangaikia tiketi za treni hiyo. Kwa mujibu wa maelezo yao ni kuwa zinasumbua kweli. Eti Kigoma mwisho wa reli, kuingia rahisi kutoka kazi, hii ni balaa. Makala ijayo itajaribu kufuatilia upatikanaji wa tiketi katika station hiyo. Hii yote kwa hisani ya Maganga Media.

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema Serikali kutoa huduma ya Elimu na Afya bure inawezekana ikiwa tu mianya ya rushwa na ufisadi itadhibitiwa ipasavyo na wananchi wataweza kunufaika na rasilimali zilizopo nchini.
Sitta alisema ni lazima turudi kwenye misingi ya uadilifu, kujali wanyonge, kukataa rushwa na kukataa ufisadi wa aina yoyote ndipo tutaweza kukusanya na kuinua uchumi wa kutosha na kulipana mishahara mizuri, kumlipa pensheni mzee na kutoa huduma hizo bure.

Aliyasema hayo alipokaribishwa katika mkutano wa akinamama wajane kutoka wilayani Karagwe na Kyelwa mkoani Kagera na kuwashirikisha wazee wa Wilaya hizo uliofanyika katika ukumbi uliopo katika ofisi za CCM wilayani Karagwe.

Sitta alisema itakuwa ndoto za kupata huduma hizo bure kama nchi haitafanikiwa kuziba mianya yote ya rushwa na wananchi wataendelea kupiga kelele wakitaka kupatiwa huduma hizo bila ya mafanikio.

“Ningependa kuwaambia wananchi, najua karibu wote tunataka utoaji wa huduma ya afya, elimu ya kuanzi msingi mpaka elimu ya juu kuwa bure, ndugu zangu katika hali ambayo hata huduma ya afya ya kawaida haipatikani ni mtihani mkubwa kwa kutoa elimu ya bure,” alisema.

Aliongeza, “Hatuwezi kuwa na nchi ina kila kitu, tunayo makaa ya mawe, maziwa, mito, bahari, madini, gesi, mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro na tuna hekta za kilimo zaidi ya milioni 88, tunataka Watanzania muamke na muache kushabikia rushwa ndogo ndogo tuingie katika utamaduni unaotuwezesha kujenga heshima ya nchi yetu kwa kujali uongozi ulionyooka na wenye uhadilifu.”

Sitta alisema wananchi wasiwe na ndoto ya maisha bora kwa kila mtanzania ikiwa rushwa na ufisadi utaendelea kutawala na kufumbiwa macho.

"Ndugu zangu hatuwezi kupata maisha bora kama kiwango cha rushwa, ufisadi na dhuluma kikiwa hivi hivi tunavyokiona hivi sasa, kwa sababu Serikali ilileta utoaji pembejeo kwa kutumia vocha sasa tutaendelea vipi kama vocha zenyewe zinachakachuliwa?" alihoji.

“Iwapo tutadhibiti mianya ya ufisadi na rushwa, nchi yetu itainuka na kuweza kuwasaidia wazee wetu, wajane, watoto yatima kwa kuwapatia huduma nyingi nzuri, ilimpadi tu ufisadi unatakiwa kupigwa vita kuanzia chini huku,” alisema Sitta.

Sitta pia aliwaomba wajane hao na wazee kupita kila mahali na kuwashaui wananchi wao wakiwemo na wana CCM kuwa makini wa watu wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa na kiserikali wasije wakafanya makosa kuwaweka watu wenye nia mbaya na nchi hii kwa kujali matumbo yao na familia zao.

“Sasa hivi hata kule bungeni mnaona baadhi ya mawaziri, anatokea mtu amekuwa waziri ndani ya miaka 2 au chini ya hapo unasikia kanunua nyumba Mikocheni ya mabilioni, haiwezekani na wala haingii akilini hakuwa waziri wa wananchi huyu ameingia kuchuma tu,” alisema.

Waziri Sitta amemaliza juzi ziara ya kiserikali ya siku tano mkoani humo alipokuwa akiangalia miradi mbalimbali inayohusiana na muingiliano wa uchumi na kijamii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
- Gazeti Mwananchi


Unaweza usielewe moja kwa moja maana ya kichwa cha habari, na kwa wale wa TUKI na BAKITA wanaweza sema kichwa cha habari kimekosewa, ingekuwa Mpenzi anauzwa! Ni kweli lakini mwandishi ametulia linauzwa akikusudia jina mpenzi na sio mtu. Fuatana nae upate alichokusudia. Ni matumaini yangu itakuwa msaada mkubwa kwako na kwa watumia mtandao wengine, jinsia zote, rika zote, matabaka yote.

Mpenzi au Dia kama lilivyotoholewa katika lugha ya Kingereza ni neno linalotumika kuitana baina ya watu wapendanao (Intimate friends or lovers). Kwa kipindi cha hivi karibuni, kutokana na kukua kwa matumizi ya Intaneti na mitandao ya kijamii, na watu wenye nia ya kujipatia utajiri kwa njia ya utapeli kupitia kwenye mtandao wameongezeka. Unaweza usielewe moja kwa moja ni jinsi gani unawasaidia au unawindwa na matapeli hao moja kwa moja au kwa njia nyingine. 

Kama unakumbuka makala iliyotangulia iliyokuwa inazungumzia “Jinsi ya kutambua akaunti za uongo zafacebook ”. Kama hukubahatika kuisoma hujachelewa. Bonyeza linki hiyo au bofya hapa uweze kuisoma. Ni kweli kuwa vitu hivyo vipo na vinakua kwa kasi kweli. Nina ushahidi wa kutosha juu ya hili. Kwa mapenzi mema na wasomaji wangu na jamii kwa ujumla nimeona ni bora tushirikishane ili msije tapeliwa. Na kwa ushahidi wa hili, siku 2 baada ya kutoa jinsi ya kutambua akaunti za uongo za facebook akaja tena ajenti mwingine kunitesti. Mtandao ni mkubwa ndani na nje ya nchi. 

Hili ni kundi la pili la mtandaoni ambapo wahusika husoma taarifa zako za facebook kasha wanakutumia meseji. Kama ni mwanaume utatumiwa meseji na mwanamke akijitambulisha na kukuomba muwasiliane nae kwa kutumia Email atakayokupa yeye na sio facebook. Kwa kuwa mtu huyo sio rafiki yako au yuko nje ya nchi, moja kwa moja meseji hiyo utaiona katika kundi la “Other Messages”Mfano wa Email hiyo umeambatanishwa hapa chini katika kielelezo namba moja.
Mfano 1:  
  • Jessy Kassala
    • Hello,
      I 'm very happy to meet you,Compliments of the day!How are you ? hope you are doing well, I am Jessy,A lovely girl,I am looking for a reliable and trusted person.I believe we can get acquainted, so if it interests you,
      Please get back to me here jessy4life0109@yahoo.co.uk so that I will send my photo to you and tell you more about my self. A good friendship is the foundation build on other relative things to come.
      NB!! please mail me in my private box not in the site OK
      (jessy4life0109@yahoo.co.uk)

      May God bless you as I wait impatiently to read from you..
      Regards,
      Jessy.
NB: HIYO AKAUNTI YA JESSY KASSALA IMESHAFUNGWA, KWA SASA AMESHAJITOA FB, AU ANATUMIA JINA JINGINE.

Utakapo mtumia anuani ya Email moja kwa moja Email ifuatayo utatumiwa ikiambatana na picha anazodai kuwa zake. Ngoja pia nikuwekee picha hizo kwa faida yako. Pia kama ni mfuatiliaji utagundua kwanza picha hizi zinajirudia kutoka mtu mmoja hadi mwingine, yaani leo unaweza ukatumiwa na anayejiita Irene kisha mwezi ujao ukatumiwa hizo hizo na mtu mwingine anayejiita Jeanne. Jambo la pili atakujengea mazingira ya kumuonea huruma. Anaweza kusema yuko Algeria, Ghana, Ivory Coast au anatoka Somalia.  

SOMA KIELELEZO CHA PILI

Hello My Dearest,
   How was your day? I believe it was fine.Mine here is very cold and like you know I am living in the refugee camp here in Dakar.In this camp Its just like one staying in the prison and I hope by Gods grace I will come out here soon.I don't have any relatives now whom I can go to as all my relatives ran away in the middle of the war.The only person I have now is Rev. Fred Maxwell who is the Rev in charge of the church (our savour de king church) here in the camp, he has been very nice to me since I came here but I am not living with him rather I live in the females hostel because the camp have two hostels one for men the other for women.

The rev; Tel number is (00221-771221690) if you call, please tell him that you want to speak with me so that he will send for me in the hostel to come and answer your Call on Mondays and Fridays of every week OK and the rev email address is (revfredmawell@ymail.com) As a refugee here I don't have any right or privilege to any thing be it money or whatever because it is against the law of this country.

I want to go back to my studies because I only attended my first year in the university before the tragic incident that lead to the death of my both parents took place.Please listen to this,I have my late father's statement of account and death certificate here with me which I will send to you later,because when he was alive he deposited some amount of money in a bank which he used my name as the next of kin,the amount in question is $6.5M(six Million five Hundred Thousand Dollars).So I will like you to help me transfer this money to your account and from it you can send some money for me to get my travelling documents and air ticket to come over to meet with you in your country. I kept this secret to people in the camp here the only person that knows about it is the Reverend because he is like a father to me.

So in the light of above I will like you to keep it to yourself and don't tell it to anyone for I am afraid of loosing my life and the money if people gets to know about it.

Remember I am giving you all this information due to the trust I want to deposit on you as a friend,I love you because you are honest and understanding man.You are truthful ,a man of vision and hardworking.I love you for been honest and truthful, I will soon be with you and possibly get married and to know you and your family then start my studies if things work out between us.

My favorite language is English.Meanwhile I will like you to call me like I said I have alot to tell you. Call me on Monday and Fridays anytime from 12 GMT.I want to hear your sweet voice of friendship and love.

Have a nice day and think about me, Awaiting to hear from you soonest
Yours Forever in mind,
Jessy.


Jambo la tatu atakutambulisha kwa mtu anayedai kuwa ni pastor wake hapo kambini anapoishi na kuwa hata mawasiliano anayotumia ni ya mchungaji huyo. Hiyo yote ni kukujengea mazingira ya kumuamini. Nia yake ni wewe uwe msaada kwake. HOJA YA MSINGI NI KUWA BABA YAKE ALIKUWA KIONGOZI SERIKALINI KATI YA NCHI ZILE ANAZOJUA KUNA MACHAFUKO YA KISIASA, NA KUWA SASA HIVI YEYE NI YATIMA KWA KUWA WAZAZI WAKE WOTE WALIUWAWA KWENYE MACHAFUKO NA YEYE NDIYE ALIYEBAKIA NA NI MKIMBIZI HIVYO KAMA MRITHI WA BABA YAKE HANA MUDA WA KUPROCESS PESA ZAKE. Hapa kwa wale wapenda pesa za haraka haraka bila kufikiria sana unaweza ukaingia mkenge. Katika transactions utatakiwa labda utume kiasi Fulani kwa njia watakayokuelekeza. 

SOMA KIELELEZO CHA 3
My Dearest,
I thank you ones again this day. I will also like to see you face to face and will use this opportunity to let you know that GOD has chosen you to help me amongst other men on earth,its now left for you and God who directed you to me to help me out from this predicament i found myself. I know you are the man i am going to depend and trust my life. I am not going to give your love to any other man because i know you will satisfy me, so needless of looking for another man.

(If you want to talk to me call with the Reverend number (00221-771221690) and tell him that you want to speak with me, he will sent for me in the hostel to come and answer you.

Please i have not told anyone except you and the rev about the existence of this money and i will like you to please keep it secret to other people because since it is (MONEY) all eyes will be on it. Remember i trust you that is why i am giving you all this information's!. My love is for you and you alone, I have informed the bank about my plans to claim this money and the only thing they told me is to look for a foreign partner who will stand on my behalf due to my refugee status and the laws of this country. You will have 15% of the total money for helping me and the remaining money will be managed by you in any business of your choice while i will continue my study.

In this regard i will like you to contact the bank immediately with this information, tell them that you are my foreign partner and that you want to know the possibilities of assisting me in transferring the ($6.5 Million US Dollars) deposited by my late father of which i am the next of kin to your account in your country.

The contact information's of the bank is as follows,
STANDARD CHARTERED BANK PLC UK.
BANK ADDRESS: NO 1 Aldermanbury Square,
London,EC2V 7SB,United Kingdom

Email address: ( standardchataredbank@bigstring.com )

The name of the transfer officer is Mr Peter Sands.
Telephone Number: +447031870528
Telephone Number: +447031864615
FAX Number: +44-87-1256-0300

Information about the deposit code are as follows.
Name of depositor:Dr. David Ellison Kassala
Nationality: Sudan
Next of kin : Miss Morin Jessy Kassala
Amount deposited: ($6.5 Million US Dollars)
Account Number: SCBUK745608902546/QB/91/A

Morin is the name my parents called me while they were alive and Jessy is the name that people and friends know me .The money is being deposited with Morin Kassala, contact them now on how to transfer the $6.5 million Dollars deposited by my late father of which i am the next of kin to your account in your country..

I have mapped out 15% for your assistance and 5% for any expenses that might come up in this transfer. My dear i am glad that God has brought you to see me out from this situation and i promise to be kind and will equally need you in every area of my life plus investing this money since i am still too young to manage this amount of money. As i told you before, this camp is just like a prison and my prayers is to move out from here as soon as possible. Please make sure that you contact the bank so that after the transfer you can send some money from that money for me to prepare my travelling documents to meet you in your country,awaiting to hear from you soonest!
Yours beloved Miss Jessy.

Kiasili inajulikana kuwa hakuna uadui kati ya mwanaume na mwanamke labda kama mwanzoni walikuwa wapenzi wakagombana. Hivyo huitumia fursa hiyo kutaka umsaidie kupprocess pesa zake for International Transactions. Mpaka kufikia hapo tayari atakutambulisha pia kwa mwanasheria. Hii ni ushahidi tosha kuwa huo ni mtandao mkubwa na hata kama watapata sh 1000/= kwako itawasaidia na ipo siku watapata zaidi. 

Hii inafanana kabisa na wale wanaotuma meseji za simu kuwa umeshinda sh mil 100, 000,000/= hivyo tuma laki moja ya kukutumia. Jaribu kufikiri na kasha uwaombe katika hizo pesa ulizoshinda wakate hata milioni 5 kwa ajili ya gharama za kutumia kasha wakutumie zinazobaki uone kama utajibiwa. Ni wakati wa kuwa macho ndugu zangu. Tuna mengi ya kufanya, hatuna muda wa kutoa pole kwa waliotapeliwa au kuibiwa kwa njia ya mtandao. Unachoweza kufanya ni kuwa makini na kila taarifa inayopita mbele zako.
HII NI FOMU YA BENK NILIYOTUMIWA NA DADA HUYO
TO
LEGAL/TRANSFER DEPARTMENT
STANDARD CHARTERED BANK PLC
NO No 1 Basinghall Avenue, London, EC2V
5DD,United Kingdom
Phones,
+447031870528 or +447031864615


Attn: Sir,
In view of your request for claims, closure and transfer of US$6.5M belonging to late Dr. David Ellison Kassala's an Sudian Nationality.

Inquiries have been made and your information coincided with the one we have in our records based on the reports before the payment verification board.

Be informed that before we can effect further transfer,we need to receive the following proofs from you to ascertain that you have been nominated by his next of kin Miss Morin Kassala.

(1) Forward a scanned copy of your identity.
(2) Present a copy of late Dr. David Ellison Kassala's certified death certificate.
(3) Present a power of attorney dull y signed an d notarized at the notary office in Senegal.
(4) Pr esent a sworn affidavit of oath/support from the high court of Senegal.

We hope that you will understand that our reque st for the above documents and informations are part of our security protocols to avoid fraudulent claims or an unwarranted taking advantage of his absence by some individuals or some other distant relations who might have had access to his privacy.
On receipts of the above documents/ informations, we shall verify them and once we are satisfied, we shall process your claim and effect the transfer.

if you have any question(s), please contact our Chief executive officer.
Mr Peter sands, email ( petersandscustomerservicescb@yahoo.co.uk) for more clarification and directives.

Regards.
Yours faithfully,
Mr Peter Sands
(Foreign /Wire Chief executive officer)

BAADA YA HIYO IKAFUATA HII HAPA KUTOKA KWA HUO MTANDAO:
Dearest Love,
How are you doing again today? l hope fine. i want to use this opportunity to thank you for your ability to help me transfer the money to your position pending my arrival to meet with you in your country to continue my education, l want you to promise me that you will not disappoint me and myself l am promising you that l will never disappoint you as well. i saw your mail and the mail of the bank and i understood the bank agreed for you to be my trustee, now about the request the bank needs from us l have with me the last statement of account and the death certificate which l will give to the lawyer when he agrees to help us so he can send them to you I thought it's the only thing the bank will need from us but since they need the power of attorney and the affidavit of oath from the high court here in Senegal .

l told the Reverend about it and he gave me the contact of this lawyer below, he is a registered lawyer in the United Nations Camp here and he is also a registered member in (Senegalaise Bar Association) who will help in preparing the documents for us. Please l will like you to contact him through email and phone today ,when you contact him tell him that you are my foreign partner and my trustee and you want him to prepare a Power of Attorney and also get the Affidavit of support from high court here in Dakar Senegal and that he will do it in your name to enable the transfer of the money to your account in Your country. His contact address are as follows,

Barr. (Dr.) Akim Mande.

Office telephone number:( +221771827005 )

Office address: 56 Ave Gorges, Dakar Senegal..

Email address: ( drbarristerakimmande@rocketmail.com )

l will like you to please contact him today for the preparation of the Power of Attorney, when contacting him i will like you to send to him your information that will be used to prepare the documents with your name in the high court, Please try and contact me when you are in contact with him and let me know if he agreed to help us, l will like you to first of all get the money transfer to your account and from it you can send some money to me to prepare my documents to come over there to meet with you over there in your country and it will be my pleasure to come over there to continue my education,i am happy that the bank agrees you to be my trustee, do have a nice day and think more of me the way i do for you,have a nice time and always think about me.
Yours forever in Love Jessy .

Kwa huo mtandao wa matapeli sio rahisi kuutambua kwani mambo mengine huwa yanakuwa ya papo kwa papo, huitaji muda wa kutafakari. Usije ukachezewa Kekundu hapo.  Kukuita MPENZI au DIA usijione kuwa wewe ndio unakismati kati ya vijana wote mtaani kwenu, na kwamba sasa ni fursa yako ya kula bata, motto kajileta mwenyewe machinjioni kumbe wewe ndio unaongozwa kwenda machinjioni. Nilimuona dada mmoja ambaye ni rafiki yangu wa facebook juu ya wall yake ameweka status inayosomeka, “Jamani sihitaji marafiki wa nje ya nchi mie”. Moja kwa moja unaelewa kuwa amepata mgeni inbox, na hivyo ameamua kuonesha hisia zake wazi wazi.

Kwa utafiti huu, nimefanikiwa kugundua mengi mno, kwa sasa kuna utafiti Fulani ninaufanya. Pindi utakapokuwa tayari nitauweka wazi kwa manufaa ya wengi. Endelea kutembelea blog yetu hii ya Maganga Media na page yetu ya facebook mara kwa mara na pindi uwapo na maswali au maoni usisite kuitumia nafasi iliyopo chini ya kila habari kwa ajili ya kuweka maoni yako. Pia unaweza kubofya hapo juu kwenye menu palipoandikwa HOME na hapo utaweza kuona habari nyingine mpya na zilizopangwa katika makundi mbalimbali na hivyo kuwa rahisi kwako kufungua ile uitakayo kwa kuclick tu na moja kwa moja utaipata. Pia endapo haijaonekana kwenye ukurasa wa kwanza haimaanishi kuwa haimo. Unaweza ukaclick heading husika kama ni ya ajira, academic, makala na kadhalika na moja kwa moja zote za aina hiyo zitakuja. Sio mwisho, pia kwa njia ya urahisi pia unaweza ukatumia SEARCH BOX juu kulia hapo kuandika KEY WORD yeyote kasha ENTER utaipata habari hiyo unayoitafuta ambayo imo ndani ya blog hii.
NI KWA NINI MATAPELI WENGI HUTUMIA PICHA ZA WANAWAKE / WAREMBO?

Kama nilivyoeleza hapo juu, kwanza ni ile hali ya kuamini kuwa mwanaume ni rahisi kushawishika kitu Fulani akifuatwa na mwanamke. Hii haikwepeki kwani hata Samsoni alidanganywa na Delila na akasema siri ya nguvu zake ambazo zilikuwa tishio kwa wafilisti. Pia Adam alidanganywa na Eva bustanini Edeni akajikuta amekula tunda la mti wa katikati ambao Mungu alimuamuru Adam asile.

Pili mwanaume anapotumiwa picha kali kama hizo ulizoziona mawazo yake yote yanahamia kwenye picha na kuwa tayari kushawishika kwa chochote anachoambiwa. Kama unabisha angalia inbox za wasichana walioko facebook ambao wameweka picha za ajabu kwangu ila kali kwao uone ni idadi ngapi ya sms zilizomo mle na kila aina ya usumbufu. Kwa ujasiri kabisa naweza nikasema hili lipo full researched na ushahidi upo. Jambo la kuzingatia wakati wewe unasoma habari hii na kugundua mbinu zao, wenyewe pia wako busy wanabuni njia nyingine zaidi ya kukuibia. Kwa taarifa yako, ile picha ya Rihana iliyokuwa ikisambaa facebook na ukiigusa tu inakuwa kama wewe ndio umeituma, imewaingizia watu pesa za kutosha. Ni kwa jinsi gani endelea kufatilia makala zetu tutakuletea. Lengo ni kutoa awareness juu ya mambo mbalimbali ya mtandaoni. 

Na mwandishi wetu wa Maganga Media kitengo cha BA Facebook


Ni mara ngapi mapenzi yamekuendesha na kutaka kuhatarisha kazi za watu au jamii au hata kuhatarisha maisha yako kwa njia moja ama nyingine? Ni kwa nini katika upendo kuna upofu fulani? Mtu unaweza kufanya jambo hatimaye ukitulia ndipo unakuja kuona hasara zake endapo lingetokea la kutokea? 

Take care. Mwana falsafa mmoja anasema kuwa jiepushe kufanya maamuzi ukiwa katika furaha sana au ukiwa katika hasira sana. Daima maamuzi yanayofanywa mtu akiwa na furaha sana au akiwa na hasira/huzuni daima huwa ni mabaya tu! Ndio pale mtu unaweza kuahidi hata kununua ndege wakati pesa tu ya kula jioni huioni mfukoni.
Katika pita pita zangu siku ya leo nikatokea Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Nilidhani kuwa shida yangu ni ndogo na labda nitaonekana mzembe sana kumbe matokeo yake yakawa tofauti kabisa. Ni kilio cha wengi, wakubwa kwa wadogo, jinsia zote. Baada ya kuwa nimehudumiwa na kuridhika na majibu ya afisa aliyekuwa kwenye kitengo hicho, nimeona nije kwenu wananchi tujadili kidogo juu ya suala hili.

Kama mada inavyosema ni upotevu wa vyeti. Nimekutana na foleni kubwa ya watu wenye tatizo la kupotelewa kwa vyeti vya kumaliza elimu ya sekondari kati ya kidato cha nne au kidato cha sita kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuibiwa au kudondosha bila kujijua.

Katika gazeti la Habari leo la tarehe 17 August, 2012 ukurasa wa 30 ambao ni maalum kwa MICHEZO/MATANGAZO kati ya matangazo yote 14 yaliyopo hapo, matangazo 9 ni ya kupotelewa na vyeti vya kidato cha nne. Na kwa mujibu wa maelezo ya dada mmoja ambaye jina lake limefanikiwa kuonekana kwenye gazeti la leo anadai kuwa foleni ni ndefu mno. Alipoulizwa ilikuwaje hadi cheti chake kikapotea anasema alikuwa anatoka kupiga photocopy, na alipofika nyumbani akagundua kuwa tayari kimepotea. Alipofuatilia hajakipata, anaamini kilipotea. Hili ni janga. 
 
Siwezi kumlaumu huyo aliyepoteza cheti kwa sababu yeyote ile, kwani hakuna anayependa hilo limtokee. Ninachotaka kujenga hoja ni juu ya madhara ya wimbi kubwa la kupotea kwa vyeti na athari zake kwa jamii yetu siku za usoni. 

Utaratibu uliopo sasa, kama mtu amepoteza cheti chake cha elimu ya sekondari kinachotolewa na NECTA, anapaswa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutoa ripoti kituo chochote cha polisi nchini, kisha kwenda kutoa tangazo la kupotelewa cheti katika magazeti ya serikali na kisha baada ya tangazo la gazetini kuchapishwa ataambatanisha hiyo taarifa ya upotevu wa cheti na nakala ya gazeti lenye tangazo lake ndipo taarifa zake za matokeo zitatumwa sehemu husika zinapotakiwa. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu, wewe uliyepoteza cheti hutapata nakala wala waraka wowote wa kuthibitisha matokeo yako wala kukutambulisha labda uendelee kutumia nakala ya cheti kama bado unayo na utakapotakiwa kutoa nakala halisi uende NECTA watatuma taarifa zako iwe kwa mwajiri au chuo kama unataka kuendelea na masomo.

Mpaka hapo, ninapata maswali manne (4) :
1. Ni kwa jinsi gani huyu mwanafunzi ataendelea kusumbuka na utaratibu huo wa kila akitaka uthibitisho asafiri kutoka huko aliko hata kama ni pembezoni mwa nchi hadi Dar es Salaam kuomba uthibitisho wake wa matokeo utumwe huko unapohitajika?

2. Ni waajiri wangapi katika kipindi hiki cha kugombania ajira ataweza kukuvumilia wewe uliyepoteza cheti utumiwe uthibitisho wa nakala yako wakati wapo watu wenye sifa kama za kwako na wana vyeti vyao halisi mkononi mwao? Endapo akikuajiri wakati anasubiria taarifa ya NECTA huoni kuwa ataundiwa tume kuwa amekula rushwa kwa kuwa umeajiriwa bila kuonesha cheti halisi?


3.     3. Kuna utaratibu gani wa kukibatilisha cheti cha awali kilichopotea na kuokotwa ambacho bila shaka kama hakijapatikana kitakuwa kinatumiwa na mtu mwingine mwenye nia mbaya? Ikiwa kwa mfano halisi kumekuwa na tabia ya mtu akipoteza simu au akiibiwa, wale walioiba simu hudiriki kuwatumia meseji watu walio kwenye orodha ya namba za simu ile kuwa, “mtumiaji wa simu hii amekufa, au kuwatapeli watu kwa kuwaomba pesa na mtumaji hutuma akiamini anamtumia mtu anayemfahamu kuwa mtumiaji wa namba ile kumbe siye.

 Katika kupambana na hilo, unapotoa taarifa ya kuibiwa au kupotelewa namba yako ya simu wafanyakazi wa mtandao husika huifunga namba. Je kwa cheti kuna utaratibu wowote?

Nilishuhudia fomu ya kujaza kwa ajili ya kuomba vitambulisho vya raia wa Tanzania zoezi lililoendeshwa jijini Dar es Salaam. Katika fomu hiyo, kwa upande wa vitambulisho kuna sehemu ya kujaza namba ya vitambulisho kama ni leseni ya udereva, cheti cha kuzaliwa, cheti cha kumaliza elimu ya sekondari, kadi ya kupigia kura, na kadharika. Je, sehemu hiyo, kwa kuwa tayari imeshawekwa, haiwezi kuwa njia mojawapo nzuri ya kutumia ili kila mtu aorodheshe namba ya vyeti vyake hapo na pindi kitambulisho kikitoka, taasisi zinazohusika na ajira wataweza kufuatilia namba za vyeti na kama mtu atakuwa amepoteza cheti chake, kwa kutaja namba yake tu yatatokea matokeo yake kama ilivyo sasa katika utaratibu unaotumiwa na TCU katika kudahili wanafunzi wa elimu ya juu?

4.     4. Ni vyeti vingapi vimerudishwa kwa waliopotelewa baada ya kutangazwa? Je ni kweli kuwa wananchi hawavioni au kuviokota? Ni kwa nini jamii isijione kuhusika katika hili ili kuwasaidia wahusika? 

Mwandishi wa makala hii hakuona umuhimu wa kuhoji upande wa pili kwa watendaji wa NECTA kwa kuwa ni hatua za awali tu hizi za kuangalia ukubwa wa tatizo na athari zake kwa jamii kupitia mjadala wa wazi, pindi taarifa ikiwa kamili utaratibu wa kuwasilisha maoni utafuatwa. Ni imani yangu kuwa NECTA wana sababu za msingi juu ya uamuzi wa kutotoa cheti wala maelezo ya matokeo kwa mtu aliyepoteza cheti isipokuwa kwa taasisi inayoyahitaji kupitia taarifa juu ya mtu husika, aliyepoteza atawasilisha maombi na matokeo yatatumwa moja kwa moja yanapotakiwa kwa gharama za muombaji.

Miongoni mwa madhara ambayo Maganga Media inaziona ni pamoja na kuwepo kwa watu wawili wanaotumia cheti kimoja katika mfumo wa ajira. Ikumbukwe kuna ajira binafsi na serikalini ambao hawatumii data base moja kutunza taarifa za wafanyakazi wao hivyo inakuwa vigumu kudhibiti suala hili

Suluhisho la kudumu ni lipi?  Karibu ndugu kuchangia mada hii. Elewa kuwa sababu za kupoteza cheti wakati mwingine inaweza kuwa ni kwa majanga au hata ajali. Ni kitu ambacho kamwe huwezi kupanga wala kudhani itatokea. Kama usivyojua siku yako ya kufa ndivyo usivyojua kesho yako. Waweza jikuta upo katika uhitaji. Nini kifanyike? 

Nawasilisha hoja.  Karibu kwenye mjadala huu: Shiriki kwa njia moja kati ya hizi unayoona ni rahisi kwako:

  1.  Tumia sehemu ya maoni iliyopo chini ya habari hii.
  2.  Facebook pages: Maganga Media na Students Resources Centre
  3.  Facebook Group: MagangaMedia                                               
  4. E – Mail: profmaganga@gmail.com