HABARI MPYA LEO  

Jinsi ya kutambua akaunti za uongo za facebook na kuwa salama

By Mhariri - Aug 5, 2012

Mtandao wa kijamii kama ilivyo kawaida ya watu wakutanapo kwa pamoja wengi hapakosi mengi, ndivyo ambavyo watu wasio na nia njema wamekuwa wakijipenyeza miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook.

Mtu anaweza kujiuliza swali iweje iwe rahisi kiasi hiki kusumbuliwa au kukutwa na uharifu wa mtandaoni kupitia akaunti yako ya facebook ambayo umeifungua kwa nia njema kabisa. Kwa faida yako unashauriwa kufuata maelekezo yaliyopendekezwa kama njia moja wapo ya kujiweka salama. Maelezo haya yatakuongoza kujua namna ya kuzigundua akaunti za uongo na kujiepusha na watu wa jinsi hiyo. Pamoja na hayo bado unaweza ukakutana na akaunti ambayo ni halisi na mtumiaji wake anafahamika, lakini sio kigezo cha kujiaminisha asilimia 100 juu ya kile unachokifanya ukiwa mtandaoni.

Kama ushauri tu, wakati wewe unafurahia huduma zipatikanazo katika mitandao ya kijamii kuna watu usiku na mchana hawalali wanawaza jinsi gani waweze kunufaika na mtandao huo huo ambao wewe unautumia. Kama unakumbuka vizuri kuna tukio lilifedhehesha watu humu facebook mwezi wa Mei na kufanya baadhi yetu akaunti zao zipotee kabisa.

Tukio lilihusu picha ya video ya Rihana, ilikuja kama link fulani, cha kushangaza kila aliyeigusa tu alionekana kuwa ndiye aliyepost picha hiyo na kutapakaa kwa marafiki zake ikiwashawishi nao kuangalia. Katika hali ya kawaida unapoona post imekuja kwa jina la rafiki yako wa karibu sana lazima tu utaiangalia. Nilipatwa na mkasa huo lakini kwa kuwa binafsi najiita BA Facebook, niliweza kukabiliana nayo.

Madhara ya akaunti zisizo halisi (Fake Facebook accounts)
Kama unajiuliza nini kitakupata kwa kuwa na rafiki wa facebook asiye na akaunti halisi, kuna baadhi ya vitu vinaweza kukusababishia hasara kwa njia moja ama nyingine. Kwa mfano unaweza kuamini kuwa mtu anakujali na kukuthamini sana kumbe nia yake ni kucheza na akili yako ili umuamini na hatimaye kupata pesa au vitu vingine kutoka kwako kama taarifa za siri na kuzitumia kuwaibia rafiki zako wa karibu.

Kuhusu usalama wa akaunti yako:
Baadhi ya watu wamekuwa wakilalamika juu ya tags za picha wasizozitaka kutoka kwa watu mbalimbali. Huna haja ya kugombana na rafiki zako au watu wote ukiwalaumu juu ya hili. Lipo ndani ya uweza wako mwenyewe. Ndani ya muda mfupi utamaliza tatizo hili kabisa. Ni kurekebisha settings za akaunti yako kwenye privacy settings na sharing. Kwa taarifa yako kama ulikuwa haujui unaweza ukachagua hata watu gani wakutumie meseji. Kuhusu tags, chagua kuwa watu wakutag kama watataka ila picha isionekane kwenye wall yako mpaka utakapo-approve wewe, unaoptions 2, kukubali au kukataa na picha haitaonekana kabisa.


MAELEKEZO NA MICHORO YA KUREKEBISHA TAARIFA ZA USALAMA KWA AJILI YA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK YATAKUIJIA HIVI PUNDE. USIKAE MBALI NA MAGANGA MEDIA. 


KAMA UNA SWALI LOLOTE LIANDIKE KWENYE SEHEMU YA MAONI CHINI YA HABARI HII ILI YAWEZE KUJIBIWA MOJA KWA MOJA AU KATIKA MAKALA ZINGINE ZITAKAZOFUATA. MAONI YAKO NI MSINGI WA MABORESHO YA HUDUMA ZETU.

CHINI YA SEHEMU YA MAONI PIA KUNA LIST YA HABARI ZINGINE UNAWEZA VUTIWA NAZO AU CLICK HOME HAPO JUU KABISA KUONA HABARI ZOTE ZILIZOMO.



HAYA TENA JINSI YA KUONDOA TAGS IMEKAMILIKA.
CLICK HERE TO READ IT.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII