AJIRA ZA UALIMU AWAMU YA PILI : Wizara ya Elimu
By Maganga Media - Mar 18, 2012
AJIRA MPYA YA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI WENYE ELIMU YA SHAHADA NA STASHAHADA MWAKA 2011/12
Kwa waombaji wote walioomba nafasi za kazi / ajira ya Ualimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambao majina yao yametangazwa katika tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI, Wanatakiwa kuripoti tarehe 19 Machi 2012 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri husika kwa ajili ya kupangiwa Vituo vya kazi. Kila mwalimu anatakiwa kwenda na VYETI vyake halisi kwenye Halmashauri alikopangwa. HAKUNA MABADILIKO YATAKAYOFANYWA. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 25 Machi 2012 atapoteza nafasi hiyo.
CHAGUA KUNDI HAPA: SHAHADA STASHAHADA
NB:
WALIMU WALIOKWISHA PANGWA AWAMU YA KWANZA AMBAO WANAOMBA KUPANGWA UPYA, MAOMBI HAYO HAYAKUKUBALIWA, WANATAKIWA WAKARIPOTI MARA MOJA KATIKA VITUO WALIVYOPANGIWA AWALI. AIDHA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI HUSIKA WAWAPOKEE NA KUWAPANGIA VITUO VYA KAZI.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII