Runinga za ‘tumbo’ kutumika hata baada ya 2012
By Maganga Media - Apr 5, 2012
Ving'amuzi kutawala huku bei ya ving'amuzi kuongezeka.
Hakutakuwa na vya bure vinahusisha matangazo yote yanayorushwa na vituo vya televisheni nchini kama TBC, ITV, Channel Ten, Star TV, DTV, Mlimani TV na nyingine nyingi zikiwemo za dini,”
MOJA ya tukio muhimu watakalokutana nalo Watanzania wakati wakikesha kuusubiri mwaka ujao 2013 ni kuzimwa kwa mitambo ya mawasiliano, inayotumia mfumo wa analogia.
Mitambo hiyo itakayoviathiri zaidi vituo vya televisheni vya kitaifa, kidini na kijamii inazimwa ili kupisha matumizi ya teknolojia mpya ya mawasiliano ya digitali.
Pamoja na mabadiliko ya teknolojia hiyo, kuzimwa kwa mitambo hiyo bila shaka kutaleta kero kwa Watanzania wengi, hasa wale watakaokutwa wakiendelea kutumia teknolojia hiyo kupata matangazo ya televisheni.
Mbali na kero ya kukosa matangazo, kuzimwa kwa mitambo hiyo kwa vyovyote vile, kutawalazimu wananchi hao bila kujali kipato chao kuingia upya mifukoni mwao ili wanunue ving’amuzi.
Ving’amuzi hivyo vilivyotengenezwa kwa teknolojia mpya ya digitali, ndivyo vitakavyowawezesha Watanzania hao kuendelea kupata matangazo ya televisheni.
Baadhi ya makampuni yaliyoshinda tenda ya usambazaji wa ving’amuzi hivyo ni Star Media (T) yenye king’amuzi cha Star Times, Agape Associates Ltd yenye king’amuzi cha Tin; na Basic Transmission Ltd.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza, itakuwaje kuhusu matumizi ya runinga zao hasa zile zenye ‘tumbo’ kwa nyuma, wanauliza itakuwaje kuhusu matumizi ya ving’amuzi vinavyorusha matangazo yake kwa satelaiti (kama vya DSTV na Zuku) na matumizi ya ving’amuzi wanavyovitumia kupata chaneli nyingi za bure, zikiwemo zote zinazorushwa hapa nchini.
Mhandisi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Andre Kisaka, anasema pamoja na mabadiliko hayo ya teknolojia, runinga zenye tumbo nyuma zinazomilikiwa na kutumiwa na Watanzania wengi, zitaendelea kutumika.
Hata hivyo ili ziweze kufanya kazi kulingana na mabadiliko hayo, wenye nazo watalazimika kununua ving’amuzi vya digitali, vitakavyokuwa na kadi zenye vipindi (chaneli) mbalimbali za televisheni.
Anasema matumizi ya ving’amuzi vya digitali yatawahusu pia wale wenye runinga zenye kioo bapa (flat screen), ambazo hazijatengenezwa kwa mfumo wa teknolojia hiyo mpya ya digitali.
Sio kweli kwamba runinga nyingi mnazoziona madukani hii leo maarufu kama flat screen, zimetengenezwa kwa mfumo wa digitali.
Nyingi zimetengenezwa kwa mfumo huo huo wa analojia kwa hiyo ili upate matangazo ya digitali, utalazimika kuwa na kinga’muzi”, Mhandisi Kisaka anasema. Anasema za digitali na vifaa vyake, vina nembo, utambulisho au taarifa inayoonesha kwamba ndani yake kuna kifaa kinachoitwa “Digital Tuner”.
Kifaa hicho ndicho kinachosaidia runinga, kunasa mawimbi yaliyorushwa katika mfumo mpya wa digitali. Anasema nembo hizo mara nyingi huandikwa Integrated Digital Tuner yaani kifaa cha digitali kimeunganishwa, au Digital Tuner Built In (Ina kifaa cha digitali ndani yake)
au Digital Receiver (kipokeo cha digitali) au DVB Tuner.
Kisaka anasema katika televisheni zingine, kuna maneno HDTV (High Definition TV) kwa maana ya runinga zenye udhahiri mkubwa. Anasema kama runinga yako, ina nembo au maneno hayo, basi unaweza kuona matangazo ya digitali bila wasiwasi wowote.
Kuhusu matumizi ya ving’amuzi vinavyorusha matangazo yake kwa kupitia satelaiti, Kisaka anasema vitaendelea kufanya kazi kama kawaida, japokuwa gharama zake zitaendelea kuwa kubwa kama zilivyo hivi sasa.
“Kwahiyo watanzania wataendelea kupata matangazo ya satelaiti kama kawaida, na watakuwa wakilipia kama wanavyolipia hivi sasa huku uwezekano wa kukosa vipindi vingi vya bure ukiwa pale pale”, anasema.
Anasema kwa watakaokuwa wakipata matangazo kupitia mfumo wa digitali, hata kama hatawakuwa na fedha za kulipia kila mwezi, wataendelea kupata vipindi vyote vinavyorushwa bure.
“Vipindi hivyo vya bure vinahusisha matangazo yote yanayorushwa na vituo vya televisheni nchini kama TBC, ITV, Channel Ten, Star TV, DTV, Mlimani TV na nyingine nyingi zikiwemo
za dini,” anasema.
Kuhusu ving’amuzi vinavyotumiwa kupata matangazo mengi ya bure, Kisaka anasema vile ambavyo havina mfumo wa digitali, havitafanya kazi tena na hivyo kuwafanya wenye navyo wakose matangazo ya televisheni.
“Watu wataweza kuona matangazo yale tu yatakayorushwa kwa mfumo wa satelaiti kupitia katika ving’amuzi hivyo”, anasema. Pamoja na mabadiliko hayo Mhandisi Kisaka anasema vituo vya redio vinavyotumia mfumo wa FM kurusha matangazo yake, vitanusurika na mabadiliko hayo, hivyo kuendelea kufanya kazi kama kawaida, kwa sababu ya ubora wa sauti zake.
Pamoja na kuondolewa hofu hiyo, Kisaka anasema serikali inakusudia kupiga marufuku uagizaji wa runinga ambazo hazijatengenezwa kwa mfumo wa digitali.
“Lengo la serikali ni kuona kwamba katika kipindi cha miaka mitano ijayo, matumizi ya runinga zilizotengenezwa kwa mfumo wa analojia yanapotea na kubakiwa na zile zilizotengenezwa katika mfumo wa digitali”, anasema.
Runinga zilizo katika mfumo wa digitali zina kioo bapa, ambazo zina tofauti kubwa na zile zenye kioo chenye tumbo au kizingo. “Kwanza runinga yenye tumbo ni nzito kuliko yenye kioo bapa, na kwa hiyo basi runinga bapa inaweza kutengenezwa kubwa bila kuwepo na ongezeko la uzito”, anasema.
Anasema runinga zenye kioo bapa, zinapunguza upotoshaji wa picha zinazorushwa kutoka katika kituo cha utangazaji, kwani ubapa huo unamfanya mtazamaji awaone watu kwenye runinga kama watu halisi waliopo ndani ya nyumba yake.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, anasema utangazaji wa digitali ni mfumo wa kurusha mtangazo, ambayo yatatoa picha na sauti nzuri. Anasema teknolojia hiyo, itawezesha pia mawimbi mengi zaidi ya picha na sauti kusafirishwa kwa
kutumia masafa madogo tofauti na teknolojia ya analojia.
“Mfumo wa utangazaji wa digitali unawezesha mifumo mingi ya picha kurushwa na vituo vya utangazaji kwa urahisi”, anasema. Anasema utaratibu wa kuhama kutoka utangazaji wa analojia kwende ule wa digitali ni makubaliano ya dunia yote chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano (ITU).
Wakati shirika hilo likitangaza kwamba nchi zote zinatakiwa ziwe zimehamia katika teknolojia hiyo ifikapo katikati ya mwaka 2015, Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), yenye nchi 12, ilikubaliana wahamie katika teknolojia hiyo ifikapo 2013.
Hata hivyo, Tanzania kwa kupitia sera yake ya mawasiliano, imeamua ihamie katika mfumo
wa digitali ifikapo saa sita usiku wa Desemba 31, mwaka huu. Mkuu wa Wilaya ya Njombe,
Sarah Dumba, anauliza ni kwa kiasi gani wananchi wameandaliwa kuipokea teknolojia hiyo.
Kama bado, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Getrude Mpaka anatoa wito kwa wizara husika na mamlaka zake, kuharakisha kutoa wa elimu ya mabadiliko hayo kabla ya siku hiyo.
“Muda uliobaki ni mdogo na kwa vyovyote vile wananchi wataendelea kuwa na maswali mengi, hivyo ni wajibu wenu kufikisha elimu hii kwa wadau na wananchi kwa ujumla”, anasema.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wanahoji sababu za Tanzania, kuharakisha kuipokea teknolojia ya digitali wakati mwisho wa matumizi ya teknolojia ya analojia ni mwaka 2015.
“Tunaambiwa kuhusu runinga za digitali, hivi upatikanaji wake ukoje na bei zake zikoje ikilinganishwa na kipato cha mtanzania wa kawaida aliyezoea kupata matangazo ya televisheni kwa kutumia antena ya runinga yake yenye tumbo nyuma,” anasema Sebius Mwenda.
Anasema kuharakisha kuingia katika teknolojia hiyo ya digitali, kutawafanya maelfu ya watanzania wanaotumia runinga zenye tumbo, kupata matangazo ya televisheni mbalimbali kwa kutumia antena za runinga hizo au zile zinazofungwa juu ya mapaa ya nyumba zao,
wakose huduma hiyo muhimu.
“Hii ina maana maelfu ya watanzania au watalazimika kununua ving’amuzi au runinga zilizotengenezwa katika mfumo wa digitali, jambo ambalo litawaongezea gharama kubwa”, anasema.
Mwenda anasema kama maandalizi yake sio ya uhakika, kwanini tuharakishe kuipokea teknolojia hiyo wakati mwisho wa matumizi ya teknolojia ya analojia ni mwaka 2015?
Swali la Mwenda halihitimishi mjadala wa mabadaliko ya teknolojia hii. Linatakiwa kuanzisha
mjadala, kama zoezi la kuharakisha kuhamia kwenye mfumo wa digitali, linaweza kuwa na athari katika haki za msingi za watu, hasa haki ya kupata habari.

CHANZO: HABARI LEO Tar 05.04.2012
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII