Mwanafunzi anajisiwa
By Maganga Media - Apr 5, 2012
POLISI mkoani Kilimanjaro inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi wa darasa la tano wa umri wa miaka 13, mkazi wa kijiji cha New Land Mvuleni. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma alisema kuwa watuhumiwa hao walimnajisi mwanafunzi huyo Aprili mosi mwaka huu saa 4 usiku huko katika kijiji hicho.
Akisimulia kisa hicho, Mwakyoma alidai kuwa mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani kwao akifuatana na dada zake wawili kwenda disko katika ukumbi uliopo nyumbani kwa mtu aitwaye Kimathi uliopo hapo New land Mvuleni. Alidai kuwa dada zake hao walikuwa wamefuatana na vijana wawili wa hapo kijijini ambao ni John Njugu na mwingine aliyetajwa kwa jina la Raymond ambao pia ni majirani zao.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Mwakyoma, wakati wakiendelea kucheza muziki katika ukumbi huo wa disko, mwanafunzi huyo alikuwa amekaa kwenye kiti akiwa na Njugu wakiendelea na maongezi kwani ni siku chache tu alikuwa amerudi kutoka Dar es Salaam.
Mwakyoma alidai kuwa baada ya muda mfupi, ilipofika majira ya saa saba usiku siku ya Aprili 2 mwaka huu, binti huyo alionekana kulewa pombe kupindukia. “Walimtoa nje ya ukumbi na kumnunulia club soda ili anywe kupunguza ulevi, lakini hakuweza kuinywa kutokana na kulewa chakari na ndipo Njugu na Raymond walimchukua na kwa nia ya kumrudisha nyumbani huku dada zake hao wawili wakibaki katika ukumbi wa disko,” alidai Kamanda.
Aliongeza kuwa baada ya kufika majira ya saa tisa, Raymond alirudi ukumbini na kuwachukua dada zake na kurudi nao nyumbani na walipofika na kufungua mlango ghafla alitoka Njugu na kuondoka kwenda kwake bila kufahamu kilichofanyika huko ndani.
Kamanda huyo alidai kuwa wakati dada zake wakiwa ndani walimsikia binti yule akilia na walipomchunguza, walimkuta amelowa damu sehemu za nyuma na mbele kuashiria kuwa alikuwa amenajisiwa na vijana hao na alipoulizwa hakuweza kusema lolote.
Binti huyo alipatiwa PF.3 na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi na hali yake bado ni mbaya na dada zake pamoja na Njugu wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.

Soma: HABARI LEO
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII