HABARI MPYA LEO  

Watuhumiwa Vurugu mutanoni Iringa wafikishwa mahakamani

By Maganga Media - May 16, 2012

Wafuasi wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakifika Kituo cha Polisi Iringa.
Washtakiwa wa kosa la kujeruhi  Ndugu Meshaki Chonanga, Alex Chonanga, Greyson Chonanga na Musa Mtete  wote kwa pamoja wakitoka Mahakamani leo baada ya kusomewa shitaka la kuwajeruhi  Ndugu Suleiman Komba, Peter Mselu na Oscar Sanga. Washtakiwa walikana kosa hilo na kesi yao kuahirishwa mpaka tarehe 25/05/2012

Washtakiwa wakishuka kwenye Karandinga kuingia rumande baada ya kukosa dhamana kutokana na wajeruhiwa  wawili kati ya wale watatu kuwa katika hali mbaya hospitali ya mkoa wodi namba 5.
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Manispaa ya Iringa wakitokea Mahakamani kuelekea Kituo cha Polisi Iringa wakienda kutaka kupata maelezo juu ya Mlalamikiwa  Mh. Diwani Idd Chonanga ambaye ndiyo mlalamikiwa wa kwanza kutofikishwa Mahakamani baada ya kukamatwa na Polisi na kuachiwa kwa dhamana.

Kaimu Kamanda wa Mkoa akiri kutofikishwa kwa Mh. Diwani Idd Chonanga mahakamani leo kwa kuwa aliachiwa kwa dhamana jana katika kituo cha Polisi na kuahidi Mh. Huyo atafikishwa mahakamani kesho tarehe 16/05/2012. Maelezo hayo alipewa Mheshimiwa Mbunge  wa Iringa Mjini Peter Msigwa (Chadema) baada ya kuonana na Kaimu Kamanda ofisini kwake leo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII