Simba yapokewa wa shangwe!
By Maganga Media - May 16, 2012
Simba iliwasili jana mchana jijini Dar es Salaam toka Sudan na kupokewa kwa mbwembwe na mashabiki wa timu hiyo, huku Kocha Cirkovic Milovan akijitetea kwa kusema wapinzani wao wamesonga mbele kwa sababu tu bahati ilidondoka upande wao.
Simba ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya , KQ315 na kupokewa na kundi kubwa la mashabiki wakiongozwa na kikundi cha matarumbeta cha Kidedea. Wekundu hao wa Msimbazi walitolewa kwa mikwaju ya penalti 9-8 na Al Ahly Shandy baada ya kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano, na hivyo kufanya matokeo kuwa 3-3. Katika mchezo wa kwanza, jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda 3-0.
Milovan aliwashukuru mashabiki wa Simba kwa kuonyesha mapenzi makubwa na sapoti ya kutosha wakati wote wa maandalizi ya mchezo huo wa marudiano na hata waliporejea. "Sikutarajia mapokezi kama haya toka kwa mashabiki, kweli hii inaonyesha mashabiki wana mapenzi na timu yao. Tumerudi bila ushindi, lakini tumepokewa kama mashujaa," alisema zaidi.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Aden Rage alisema makosa matatu waliyofanya katika mchezo huo yamewagharimu na wanayakubali matokeo na hivi sasa mtazamo wao ni katika mechi zaidi za kimataifa. "Hivi sasa tunaiangalia michuano, mapokezi tuliyopewa yanaonyesha ni jinsi gani washabiki wetu walivyo watu wa mpira," alisema Rage.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII