Majeshi kuwashtaki waliofoji vyeti
By Maganga Media - May 16, 2012
SIKU moja baada ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), kueleza kwamba askari zaidi ya 948 wamegundulika kutumia vyeti vyenye majina yanayofanana na waajiriwa wengine serikalini Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi wamesema wanajipanga kuifanyia kazi taarifa hiyo kwa gharama zozote.
Juzi, Nida ilitoa taarifa ikionyesha udanganyifu wa vyeti vya elimu JWTZ na polisi na kuonya ni moja ya changamoto zinazoukabili mchakato mzima wa utoaji wa vitambulisho hivyo. Jana kwa nyakati tofauti, JWTZ na Polisi walitoa tamko na kusema watachunguza kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) na Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Nida na watakaobanika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema uamuzi huo umekuja baada ya Nida kutoa taarifa ya kuwepo kwa wanajeshi 248 walioghushi vyeti hiyo na kujiunga na jeshi. Alisema kitendo hicho ni kinyume na sheria na kwamba mwanajeshi atakayebainika amefanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kushtakiwa kwenye mahakama za kijeshi na uchunguzi ukikamilika na ikatokea amethibitika kughushi, atafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wake, polisi wametoa taarifa kwa umma na kusema baada ya kusikia taarifa hiyo ya Nida, imeunda timu maalumu itakayofuatilia suala hilo kwa karibu zaidi na kuchukua hatua zinazostahili. Taarifa iliyotolewa jana na jeshi hilo na kusainiwa na msemaji wake, Advera Senso imesema baada ya kuipokea taarifa hiyo, limeunda timu maalumu kutoka makao makuu ya polisi itakayowahusisha maofisa mbalimbali.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII