Hollande aapishwa
By Maganga Media - May 16, 2012
Francois Hollande ametawazwa kama rais mpya wa Ufaransa, na kumfanya kuwa rais wa kwanza wa kisosholisti kuapishwa katika miaka kumi na saba.Bwana Hollande alisema kuwa anafahamu vyema changamoto ambazo Ufaransa inakabiliana nazo ikiwemo, madeni na uchumi unaojikokota. Baadaye hii leo rais Hollande atamteua waziri mkuu na kisha kwenda nchini Ujerumani kwa mazungumzo na Chansella Angela Merkel kufanya mazungumzo zaidi kuhusu mpango wa Ujerumani wa kutafuta suluhu kwa mgogoro wa kiuchumi unaokumba bara la Ulaya.
Hapo jana thamani ya Euro ilishuka masoko ya hisa nayo yakishuka huku hali ya kisiasa nchini Ugiriki ikiendelea kuwa tete. Mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa fedha wa ulaya, Jean-Claude Juncker, alisisitiza hapo jana kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Ugiriki inasalia katika muungano wa Ulaya.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII