Hoteli yashambuliwa na magaidi Mombasa
By Maganga Media - May 16, 2012
Hoteli moja maarufu visiwani Mombasa imeshambuliwa kwa maguruneti na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Hoteli hiyo ,Bella Vista Restaurant,ni maarufu sana kwa watalii na wenyeji na iko kando ya barabara kuu itokayo bandari ya Mombasa. Mkuu wa kitengo cha polisi wa jinai mjini Mombasa Bwana Ambrose Munyasya amesema kuwa watu watano walijeruhiwa vibaya katika kisa hicho. Uchunguzi wao wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na milipuko mitatu katika klabu hicho cha Bella Vista Restaurant.
Inadaiwa kuwa watu wawili walikwenda katika Klabu hicho wakitaka kuruhusiwa kuingia.
Lakini walipotakiwa kupekeliwa na maaskari wa hoteli hiyo walikataa na ndipo wakarusha maguruneti hayo.
Walioshuhudia mkasa huo wanasema kuwa magaidi hao walifyatua risasi ovyo ovyo wakati walipokuwa wakitoroka. Hata hivyo polisi wanasema hawaja mkamata mtu yeyote kutokana na kisa hicho.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII