Ndege ya ATCL yaanguka
By Maganga Media - Apr 10, 2012
WATU 39 waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kutoka Kigoma kuelekea Tabora na baadaye Dar es Salaam, wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria aina ya Dash 8 Q300 kushindwa kuruka na kuingia porini.
Ndege hiyo namba 5H - MWG iliyokuwa na mruko namba TC 119, ilivunjika vipande kadhaa kabla ya zimamoto kufika kudhibiti uwezekano wa kuteketea kwa moto.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athumani Mfutakamba alisema ndege hiyo ilikuwa na abiria 35 na wafanyakazi wanne.
“Wote wametoka kwenye ndege hiyo wakiwa salama na wamepelekwa hotelini Kigoma wakati ATCL ikifanya mpango wa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam,” alisema Mfutakamba.
Hata hivyo, Naibu Waziri huyo hakueleza chanzo cha ajali hiyo kwa maelezo kwamba uchunguzi bado unaendelea.
Lakini Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kihenya Kihenya alisema chanzo cha ajali hiyo ni ndege kushindwa kuruka na kuacha njia kisha kuingia porini.
Alisema sababu za kushindwa kuruka, zilitokana na matope yaliyokuwa yametapakaa katika eneo hilo la kiwanja kiasi cha kuifanya ipoteze mwelekeo.“Ilivutwa pembeni kutokana na njia ya kurukia kuwa na matope na ndiyo maana ilipoteza mwelekeo wake wa kawaida. Hali hiyo imesababisha bawa moja la upande wa kulia kukatika kabisa, lakini wasafiri wote wametoka salama na hakuna hata mmoja aliyekufa.”

Ndege hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Kapteni Emmanuel Mshana akiwa na msaidizi wake, Mbwali Masesa.
Hii ni ajali ya pili kutokea katika uwanja huo katika kipindi cha miaka sita baada ya mwaka 2006 ndege ya Umoja wa Mataifa (UN) aina ya Boing 737 iliyokuwa ikitoka DRC ikuanguka.
Aidha, ni ajali ya pili kwa ndege za ATCL katika kipindi cha miaka miwili baada ya ile ya Februari 2010, ambayo abiria 40 walinusurika kufa baada ya ndege yake aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kupata ajali wakati ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Chanzo cha ajali hiyo kilielezwa kuwa ni ndege hiyo kuacha njia na kusababisha tairi za mbele kung’oka kabla ya kusimama nje ya barabara yake ya kawaida.
ATCL iliyoanzishwa baada ya lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mwaka 2002.

ATC ni moja ya mashirika ya ndege yaliyoonyesha kukua kwa kasi miaka ya 1980 na 1990 lakini lilianza kuyumba kutokana na uendeshaji mbovu na hali ikawa mbaya zaidi baada ya kuingia ubia na SAA na ilivunja mkataba huo Septemba 2006 baada ya kubaini kuwa ATCL inazidi kudidimia.
Hali ya ndege inavyoonekana upande wa kushoto.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII