HABARI MPYA LEO  

Mwenye hatma ya Lulu ni DPP

By Maganga Media - Apr 10, 2012

MSANII Elizabeth Michael (Lulu)

HATMA ya msanii maarufu wa kike Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’ anayeshikiliwa polisi kufuatia kifo cha msanii Steven Kanumba iko mikononi mwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Inasemekana kuwa uvumi uliokuwepo juu ya Lulu kumsukuma au kumpiga Kanumba si kweli,kwani madaktari wamegundua kuwa alishtuka ubongo ukatingishika na ndilo jambo lililosababisha kifo chake baada ya kushindwa kupumua.Tutawaletea habari kamili tukithibitisha kutoka vyanzo rasmi. Msaidizi wa Mwenyekiti,Dar

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema suala la msanii huyo kusema ana kesi ya kujibu au la, liko mikononi mwa DDP ambaye ndiye atakayepitia jalada baada ya polisi kukamilisha upelelezi wao.

Kamanda Kenyela alisema Lulu kupelekwa mahakamani ni uamuzi wa DPP ambaye atatakiwa kulipitia faili lake na kujiridhisha kama ana kesi ya kujibu au la.  “Kumpeleka mahakamani ni mpaka DPP tutakapomwasilishia jalada la tuliyoyakusanya na ndiye atakayeamua kama kuna kesi ya kujibu au hakuna,”alisema Kamanda Kenyela. 

TAMWA YATAKA LULU ATENDEWE HAKI
MKURUGENZI wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya, ametaka kufanyika uchunguzi huru wa kina kuhusiana na kifo cha msanii wa filamu nchini, Steven Kanumba, ili kumtendea haki Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayedaiwa alikuwa naye muda mfupi kabla mauti kumfika.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nkya alisema uchunguzi huru unahitajika kutokana na ukweli kuwa, tukio hilo limetokea chumbani tena wakiwa wawili (Kanumba na Lulu) na kutaka jamii kuachia polisi ifanye kazi yake.

Nkya alisema kitendo cha baadhi ya watu kumlaumu Lulu kuwa ndiye amesababisha kifo cha Kanumba, hakina maana na iwapo kauli kama hizo zitaendekezwa zinaweza kuathiri uchunguzi huo.

Pia, aliwataka ndugu, jamaa na marafiki zake kushikamana kipindi hiki cha msiba wakati wanasubiri uchunguzi wa polisi.
“Siyo vizuri kuanza kulaumiana, tuwaache polisi watimize wajibu wao kwani kuna vitu vingi vya kuangalia ikiwamo kujua kilichosababisha kifo chake ni kipigo au jereha ambalo lilitokana na kuanguka na alianguka kutokana na nini hadi kutoa povu mdomoni,” alisema.

MJENGWA AULIZA
"Je, Ni Nani Anayemfariji Msichana Huyu Wa Miaka 18 Aliyeondokewa Na Mpenzi Wake. Na ukweli unabaki, kuwa Lulu ni mwanadamu kama wewe na mimi. Na kwa yote yaliyotokea, anabaki kuwa ameondokewa na mpenzi wake. Je, ni nani anayemfariji msichana huyu wa miaka 18 aliyeondokewa na mpenzi wake?"

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Aomboleza Msiba Wa Kanumba

 

Msanii Wa Filamu Wema Sepetu Kwenye Msiba Wa Kanumba

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII