HABARI MPYA LEO  

NCHUNGA 'AFUNIKA KOMBE' KIAINA

By Maganga Media - May 13, 2012


MWENYEKITI wa Yanga Lloyd Nchunga (Pichani) amenyamazisha kimtindo kelele za wanachama wa klabu hiyo wakliokuwa wakimshinikiza kuachia ngazi kutokana na timu hiyo kufanya vibaya kwenye msimu uliomalizika wa ligi kuu soka Tanzania bara na hatimaye kupokwa ubingwa. Pamoja na kupokwa ubingwa huo uliokwenda kwa mahasimu wao wa jadi Simba, Yanga ilijikuta katika machungu mengine walipopigwa mabao 5-0 na Simba katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara na hivyo kufanya wanachama wa Yanga na hasa wazee kuendeleza shinikizo la kutaka ajiulu kwani walishabaini hali mbaya kwa timu hiyo na kuitaka kuichukua timu lakini Nchunga aliwageuka na kusema hawezi kutoa timu kwa wahuni. 
Nchunga baada ya kuketi  na kamati ya utendaji ya Yanga na kujadili masuala mbalimbali, amewaambia waandishi wa habari mchana wa jana kwamba wameachana na masuala ya kufanya kwao vibaya kwenye ligi na sasa wanaangalia mbele. 
Alisema kamati ya utendaji imeipa idhini kamati ya usajili kusaka wachezaji wazuri ambao wataitunmikia timu hiyo kwenye michuano ya Kagame mwaka huu na hatimaye kutetea ubingwa wake.
 
 Kama hiyo haitoshi, Nchunga amesema mkutanoi mkuu wa Wanachama unatarajiwa kufanyika Julai 15 hivyo amewataka wanachma kulipia adha zao ili kupata haki yao ya kimsingi ya kushiriki kwenye mkutano huo. Aidha, Nchunga alisema Mei 20 anatarajiwa kukutana na wazee wa baraza wa klabu hiyo wa mkoa wa Dar es salaam huku akiwaomba wazee wa mikoa mingine watakaoweza kushiriki kuhudhuria.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII