HABARI MPYA LEO  

LOWASA Ulitatuaje tatizo la Ajira kwa vijana?

By Maganga Media - Mar 23, 2012

Waziri mkuu aliyejiuzuru, Edward Lowassa

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amemtaka Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kueleza jinsi alivyoshughulikia kutatua tatizo la ajira wakati akiwa Waziri Mkuu. Kauli hiyo ya Nnauye inakuja siku moja baada ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka kueleza kwamba tatizo hilo haliwezi kufafanishwa na bomu na kufafanua kuwa wanaosambaza uvumi huo hawaitendei haki Serikali.

“Kila siku wanalalamika Serikali ya CCM inatengeneza bomu katika suala la ajira, lakini hao wanaolalamika si walikuamo madarakani na  walifanya nini. “Unapofika wakati unazungumzia masuala yanayogusa jamii na Taifa kwa ujumla unapaswa kuwa na  uhakikika na unachokisema sio kupita katika makanisa kuongea kitu ambacho huna uhakika. “Amekuwa akitumia njia mbalimbali hususan makanisani kuelezea tatizo la ajira ambalo linaitatiza serikali, lakini mimi nabaki na msimamo ule ule kuwa  yeye alipokuwa serikalini (Waziri Mkuu) alifanya nini kutatua tatizo la ajira,” alihoji tena.

Tucta
Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi (Tucta), Nicolas Mgaya alisema suala la ajira bado ni tatizo  kwa serikali na kwamba linapaswa kutatuliwa. Mgaya alisema kuna vijana wengi wanahitimu masomo katika kila fani kwamba kupata kazi ni tatizo ambalo kama litasimamiwa ipasavyo litapungua.

Mgaya alisema serikalini kuna upungufu wa wafanyakazi, lakini inashindwa kuajiri,  sasa umefika wakati wa kuziba mapengo hayo na kuwaondoa vijana walioko mitaani bila ajira. “Katika shule za msingi na sekondari kuna upungufu wa walimu, lakini majumbani kwetu kuna vijana waliohitimu masomo ya ualimu hawajaajiriwa sasa hapa serikali inataka kutatua ama inaongeza matatizo,” alihoji Mgaya.

CHANZO: Mwananchi

Maganga Media

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII