Bajeti ya Serikali yapita!
By Unknown - Jun 24, 2012
WAZIRI wa Fedha, Dk. William Mgimwa ‘amewakuna’ wabunge wa Bunge la Tanzania baada ya kuwajulisha kuwa Serikali imekubali mapendekezo yao mengi waliyotoa wakati wanachangia bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Dk. Mgimwa amelieleza Bunge kuwa, uamuzi huo wa Serikali utawawezesha wafanyabiasha wadogo wakiwemo waendesha ‘bodaboda’ kujiendeleza kibiashara.Serikali yetu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu…Serikali ni sikivu kwa wabunge wote” amesema Dk. Mgimwa wakati anajibu hoja za wabunge waliochangia bajeti hiyo.
“Lakini Serikali imekubali mapendekezo ya waheshimwa wabunge” amesema. Kwa mujib wa Waziri Mgimwa, Serikali kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa viwanda vinavyozalisha nguo kwa kutumia pamba inayolimwa nchini. “Tumeikubali hiyo hoja, tunaifanyia kazi” amelieleza Bunge na kubainisha kwamba, uamuzi huo utasaidia kuongeza ajira nchini na mapato ya wananchi.
Amesema, Serikali inafanya uchambuzi wa suala hilo ili kuona ni wapi itafidia , nakwamba, itatoa ufafanuzi wa jambo hilo katika Muswada wa Fedha wakati wa Mkutano unaoendelea wa Bunge mjini Dodoma.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII