HABARI MPYA LEO  

AY na Mwana FA wafunika BBA

By Unknown - Jun 24, 2012

Gumzo lililoachwa katika jumba la Big Brother mwishoni mwa wiki iliyopita ni kuhusiana na Mwanamuziki Ambwene Yesaya kutoka Tanzania aliyealikwa kwenda kupiga onesho moja la kimataifa katika sherehe za kuwaaga washiriki jessica na Liz ambao walitoka kwenye jumba hilo.

Onesho lilitangazwa kwamba litamhusisha mwanamuziki AY kutoka Tanzania lakini alipoibuka na swahiba yake ambaye walikuwa wote tangu enzi za East Coast na kupiga MegaMix ya nguvu huku kila mtu akifurahi na nafsi yake.

Nyimbo walizoimba wasanii hao wa muda mrefu katika tasnia ya muziki wa Bongoflava ilihusisha nyimbo zao zote maarufu ambazo waliimba pamoja kama Ngoja Ageuke, habari Ndio hiyo, Dakika moja, Safi hiyo ambazo ukiweka suala la lugha yake kutoeleweka, zilionekana wazi wazi kukonga nyoyo sa mashabiki wa shindano la Big Brother ambao walihudhuria sherehe hizo za kuaga washiriki zinazofanyika kila mwisho wa wiki, siku ya Jumapili8.

Wasanii hao walirejea juzi kutoka Afrika ya kusini na usiku wa leo (Jumapili), mwana FA anatarajiwa kumsindikiza Linah kwenye onesho lake la kuzindua wimbo wake mpya aliomshirikisha AJ Ubao iliyorekodiwa nchini Marekani inayokwenda kwa jina la All I need.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII