HABARI MPYA LEO  

Wabunge wa Zimbabwe watahiriwa kupunguza HIV

By Unknown - Jun 24, 2012

Wabunge karibu 10 nchini Zimbabwe wametahiriwa kama moja wapo ya hatua zao ya kukabiliana na kusambaa kwa virisi vya Ukimwi nchini humo

Nje ya majengo ya bunge mjini Harare , kulijengwa zahanati ndogo kwa sababu ya shuhuli hizo za kuwapasha wabunge tohara. Blessing Chebundo, ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wanaopambana na Ukimwi amesema nia yake hasa ya yeye kuamua kupashwa tohara ni kuchochea wanaume nchini Zimbabwe kutairiwa. Bwana Chebundo anasema kuna wabunge zaidi ya 120 na wafanyikazi wa bungeni ambao wameonyesha nia yao ya kutahiriwa.

Shirika la afya duniani WHO linasema kupasha tohara kunapunguza atari ya wanaume kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60.

Zimbabwe ni moja wapo wa mataifa 13 barani Afrika ambapo mwaka wa 2007 shirika la WHO inasema kuna haja kubwa ya kuanzisha harakati za kuwatahiri wanaume. Jana, wabunge hao walijitokeza hadharani ili kupimwa hali yao ya Ukimwi.

Wabunge hao wanachochea wanaume nchini Zimbabwe kukubali kutahiriwa, kama njia mojawapo ya kupumguzu maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hii nikutokana na takwimu za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa karibu robo ya wanaume wote nchini Zimbabwe wameambukizxwa virusi.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII