HABARI MPYA LEO  

Kanumba na Lulu feki jijini!

By Maganga Media - Jun 10, 2012

 
Gumzo limetanda jijini siku chache baada ya kifo cha aliyekuwa mwigizaji nguli, Steven Charles Kanumba ‘The Great’ huku mpenzi wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa Segerea, Dar kuhusiana na kifo hicho, mtaani wameibuka watu wawili wanaofanana na mastaa hao na kusababisha gumzo kubwa.

Taarifa zilieleza kuwa kuna binti aliyetajwa kwa jina la Yolanda Michael (Lulu fotokopi, pichani), mkazi wa Tip Top jijini Dar ambaye amefanana na Lulu na amekuwa akipata wakati mgumu anapokatiza mitaani akihisiwa ni Lulu halisi.
 

“Kama mtakumbuka siku ya mazishi ya Kanumba kuna msichana aliyenusurika kichapo, basi ni mimi na siyo siku hiyo tu, hakuna kipindi cha maisha yangu ambacho niliishi kwa tabu kama baada ya kifo cha Kanumba,” alisema Yolanda mwenye ndoto ya kuwa mwigizaji mkubwa.
 

Mbali na kufanana umbile, pia Yolanda anafanana na Lulu orijino kuanzia pua, macho, midomo na sehemu mbalimbali za mwili. Pia, jina la baba yake ni Michael kama lilivyo la baba wa Lulu orijino (Michael).

Akizungumza na paparazi wetu katika ofisi za gazeti hili, Thadei Pius Michael (jina kama la baba Lulu na Yolanda), ambaye ukimuoana huulizi kwa jinsi alivyofanana na marehemu Kanumba, amekuwa akipata wakati mgumu kwa watu wanaopita katika eneo lake la kazi ya ufundi gereji.
 
“Hata kabla ya kifo cha Kanumba, watu wengi walikuwa wakiniambia kwamba wakidhani ni Kanumba waliponiona,” alisema kijana huyo mpole anapozungumza na kuongeza: “Baada ya kifo cha Kanumba ndiyo hali imekuwa mbaya zaidi kwani watu wakiniona wanadhani ni mzimu wa marehemu Kanumba.  “Wengine wamekuwa wakinizunguka na kunikagua kwa kunitazama hali ambayo inanikosesha amani.”
Baadhi ya watu walidai walishindwa kuamini kutokana na jamaa alivyofanana na The Great kuanzia midomo, macho, pua, urefu na baadhi ya sehemu nyingine za mwili.
Wakati Yolanda akiendelea kuzua gumzo, Tadei Pius (Kanumba fotokopi), naye mkazi wa Dar amekuwa akileta songombingo la aina yake kwa mashabiki wa marehemu Kanumba ambao wakimuona hudai kuwa kumbe The Great hajafa kutokana na kufanana kwao.

Akihojiwa ‘exclusively’ na mapaparazi wetu wa gazeti la Risasi, Yolanda, binti wa miaka 18 aliweka wazi kuwa mara kadhaa amenusurika vipigo kutoka kwa watu ambao walitaka kumuadabisha wakidai kuwa yeye ni Lulu (Elizaberth Michael) wakimtuhumu kwa kifo cha Kanumba.
 
“Ama kweli duniani wawiliwawili, najua Mungu ana makusudi yake kwa sababu haiwezekani wakafanana kwa kiasi hiki,” alisema Dullah, mkazi wa Dar.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII