HABARI MPYA LEO  

Ajali ya Helkopta yaua mawaziri Kenya!

By Maganga Media - Jun 10, 2012

Imethibitishwa kuwa Waziri wa usalama wa taifa wa Kenya George Saitoti pamoja na msaidizi wake Joshua Ojode ni miongoni mwa watu saba waliofariki dunia kwenye ajali ya helicopter ya Polisi iliyotokea kati ya saa tatu au saa tano leo asubuhi huko Ngong Kenya. Chanzo cha ajali ni kutokana na hali mbaya ya hewa ambapo helicopter hiyo ilikua na marubani wawili akiwemo mmoja wa kike.

.
Waziri wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Waziri Saitoti

Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.

Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania  kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong. Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.

Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Waliofika kwenye eneo la tukio.
.
.
.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII