Uzinduzi Vitambulisho vya Taifa wasitishwa
By Maganga Media - May 15, 2012
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa Bw.Dickson Maimu Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari waandamizi leo makao makuu ya mamlaka ya vitambulisho vya Taifa jijini Dar es salaam, kuhusu kusitishwa kwa muda wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho vya Taifa uliokuwa ufanyike mapema mwezi huu, ili kuyafanyia kazi mapendekezo ya wadau yaweze kuingia kwenye mfumo.hata, Hivyo Bw.Dickson Maimu amesema mradi umekamilika ila zimejitokeza changamoto na mahitaji ya msingi kutoka kwa wadau muhimu wa vitambulisho vya Taifa kwa hiyo mamlaka haina budi kuyafanyia kazi ili kitambulisho kiwe kimekidhi maitaji yote ya msingi.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo leo katika makao makuu ya mamlaka ya vitambulisho vya taifa jijini Dar es salaam.
(PICHA NA PHILEMONI SOLOMON)
(PICHA NA PHILEMONI SOLOMON)
“Katika uzoefu tuliopata katika majaribio ya utoaji vitambulisho, tumebaini baadhi ya waombaji ambao wameonekana kutumia vyeti visivyo vyao, hivyo tumeona kuwapo haja ya kuwa na chombo maalumu cha uchunguzi, ili kujihakikishia kunakuwa na taarifa sahihi,” alisema Maimu.
Kuhusu kuchelewa kutoa vitambulisho hivyo, alisema kulitokana na mabadiliko makubwa katika mfumo wa daftari la kielektroni la anuani za makazi na simbo za posta na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Lakini wakati tunaendelea na utekelezaji huu, kumekuwa na mabadiliko ya majina ya mikoa, wilaya, kata na vijiji, kutokana na uamuzi wa Serikali kufanya marekebisho katika Serikali za Mitaa, kwa kuongeza mikoa mipya ambayo haikuwapo wakati tunasaini mkataba na mkandarasi,” alisema.
Kutokana na changamoto hizo, alisema Mamlaka hiyo imeona ni busara kuzindua mradi ukiwa tayari umetatua changamoto hizo jambo ambalo litachukua zaidi ya miezi miwili au pungufu. Sababu nyingine ya kuchelewa kwa vitambulisho hivyo kwa mujibu wa Maimu ni kufanya usajili wa pamoja na NEC.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII