HABARI MPYA LEO  

Mbunge atishiwa kuuawa!

By Maganga Media - May 15, 2012

Oscar Sanga alijeruhiwa juzi kwa mapanga akiwa kwenye mkutano wa Chadema ambapo hata mbunge wa Iringa Mjini Mh.Peter Msigwa alinusurika.amelazwa hospitali ya mkoa Iringa na anaendelea vizuri

VUGUVUGU la kisiasa katika jimbo la Iringa mjini, limezidi kupanda joto baada ya Mbunge wa jimbo hilo, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa kudai kuwa ametishiwa kuuawa kwa maneno na Diwani wa kata ya Nduli, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamis Chonanga.

Hatua ya mbunge kudaiwa kutishiwa kuuawa imemfanya mbunge huyo kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha Iringa mjini.

Hali hiyo inatokana na vurugu za kisiasa zilizotokea juzi katika mkutano wa hadhara wa Chadema, uliofanyikia kata ya Nduli, ambao ulisababisha baadhi ya vijana kumvamia Mchungaji Msigwa wakitaka kumcharanga mapanga na kusababisha majeraha kwa vijana watatu wa Chadema.

Katika mkutano huo, Mchungaji Msigwa alinusurika kucharangwa mapanga baada ya kundi la vijana wanaoaminika kutokea CCM  kumvamia kwa madai ya kukerwa na kundi la watu zaidi ya 90 akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji, Ayubu Mwenda kuamua kujiunga na chama hicho. Waliojeruhiwa huku mmoja wao akilazwa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa, Wodi namba tano ni Oscar Sanga, Perter Mselu na Saleh Komba.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII