HABARI MPYA LEO  

Precision Air yadhamini 'AIESEC Career Fair' chuo cha SAUT jijini mwanza

By Maganga Media - May 15, 2012

Meneja Mauzo wa PrecisionAir Kanda ya Ziwa Bw. Eliud Mwasongwe akielezea kuhusu kampuni ya ndege ya PrecisionAir pamoja na sera zake kwa ajira kwa vijana katika siku ya ‘Career Fair’ iliyoandaliwa na asasi ya AIESEC chuoni SAUT.
Mkurugenzi Mkuu wa MAANISHA! Bw. Andrew Mahiga (katikati) ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo akitoa cheti cha ushiriki kwa Meneja Mauzo wa PrecisionAir Kanda ya Ziwa Bw. Eliud Mwasongwe. Akiwatazama ni Rais wa AIESEC SAUT Bw. Heri Emmanuel.
Meneja Mauzo wa kanda ya Ziwa kutoka PrecisionAir Bw. Eliud Mwasongwe akitoa ufafanuzi juu ya huduma za shirika hilo la ndege kwa baadhi ya wanafunzi wa SAUT waliofika bandani hapo.
Afisa Mawasiliano wa PrecisionAir Amani Nkurlu (kulia) ambaye pia aliwahi kuwa Rais wa AIESEC SAUT 2009/2010 akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa MAANISHA! Andrew Mahiga (wa pili kushoto) na wanachama wa AIESEC SAUT walipotembelea banda la kampuni hiyo.
Wanafunzi wakishiriki katika siku ya 'Career Fair' chuoni SAUT iliyodhaminiwa na PrecisionAir.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII