HABARI MPYA LEO  

Udom kujenga viwanja vyenye ubora

By Maganga Media - May 14, 2012

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa bonanza la Kikula Sports Day likiendelea hapo jana katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu Cha Dodoma vilivyopo Katika Kitivo Cha Sayansi ya Jamii.
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kina mpango wa kujenga viwanja vya michezo vyenye ubora ili kuweza kukaribisha timu mbalimbali.

Hayo yalisemwa juzi na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula wakati wa bonanza la michezo la Profesa Kikula lililofanyika katika chuo hicho mwishoni mwa wiki na kuoingeza kuwa mwaka huu chuo hicho kimefanikiwa kujenga viwanja vipya vya michezo na kilichobaki ni kuwekwa kwa chokaa.

"Michezo ni muhimu sana kwa wanafunzi, tutajitahidi kuwa na viwanja vingi ili wanafunzi wengi zaidi washiriki katika michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, pete, mpira wa wavu, na michezo mingine," alisema

Alisema kuwa bonanza la mwaka huu limekuwa na mwamko mkubwa tofauti na mwaka uliopita kwani wengi wamejitokeza kushiriki mashindano hayo na kuwataka wanafunzi kuwa na tabia ya kushiriki katika michezo mbalimbali kwa lengo la kujenga uhusiano mwema na kuimarisha afya .

Mkufunzi wa michezo wa chuo hicho, Patrick Mwani alisema kuwa changamoto wanayokabiliana nayo ni upungufu wa vifaa vya michezo kutokana na chuo hicho kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanashiriki michezo.

Katika bonanza hilo, wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho walishiriki michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, netiboli, mbio za meta 100, mbio za magunia, kufukuza kuku na kuvuta kamba.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII