Bonanza la UDOM Lafana!
By Maganga Media - May 14, 2012
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa bonanza la Kikula Sports Day likiendelea hapo jana katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu Cha Dodoma vilivyopo Katika Kitivo Cha Sayansi ya Jamii.
Wadada waliojitokeza Kwenye Shindano la Kula katika bonanza hilo lililofanyika jana katika viwanja vya kitivo Cha Sayansi ya Jamii.
Washiriki wa Shindano la Kula Hao wakiendelea kushindana Kula katika Bonanza la Kikula Sports Day lililofanyika Jana katika Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma
Zoezi la Ushindani Wa Kula likiendelea hapo
Mshindi wa Shindano la Kula aliyeshikwa mkono akionyeshwa kuwa ndie mshindi wa kula katika bonanza hilo lililofanyika jana katika viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma ambapo lilidhaminiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idris Kikula pamoja na Kampuni ya Vinywaji Ya Coca Cola
Prof Idris Kikula (Katikati) akitabasamu wakati mchezo wa kukimbiza kuku kwa wafanyakazi ukiendelea katika bonanza lililofanyika jana Katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Meneja Wa Kampuni Ya Coca Cola Kanda ya Kati Dodoma Bwana Maginga Akitoa Shukrani ka Uongozi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Na Vilevile Ndio KAmpuni iliyodhamini bonanza hilo Na Hapo alikua akikabidhi Zawadi Za Kreti za Soda kwa Uongozi Wa Chuo Kwaajili ya Kukabidhi kwa Washindi Wa Michezo Mbalimbali
Msanii Chipukizi Chipoka akitoa burudani katika bonanza hilo lililofanyika jana katika Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Tukibadilishana Mawazo na Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)Prof Idris Kikula (Wa pili Kulia), Wa Kwanza Kulia Ni Mmiliki na Mwandaaji Wa Mtandao Huu Wa Lukaza Blogu Bwana Josephat Lukaza, Wa Kwanza Kushoto Ni Kijana Abdul na Wa pili Kushoto Ni Mkuu wa Masomo ya Shahada ya Kwanza Prof Msofe tulipokutana Jana Katika Bonanza La Kikula Sports Day
Baadhi ya Wanafunzi Waliojitokeza Kutazama na Kushuhudia Bonanza Hilo lililofanyika Jana KAtika Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambapo bonanza hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Coca Cola pamoja na Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula.Picha Zote Kwa Hisani ya Lukazablog
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII