MSHINDI WA MIL 10 ZA VODACOM
By Maganga Media - Apr 16, 2012
Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo kubwa ya mwezi ya kumpata mshindi wa milioni 10 wa promosheni ya M-PESA, ambapo mkazi wa Kitangiri mkoani Mwanza, Revocatus Mkama amejishindia fedha hizo, jumla ya sh. milioni 300 zimetolewa kwa washindi wa promosheni hiyo tangu kuchezeshwa. Kulia ni Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom, Reenu Verma.
Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akionesha nambari ya Mshindi wa droo kubwa ya mwezi ya kumpata mshindi wa milioni 10 wa promosheni ya M-PESA, ambapo mkazi wa Kitangiri mkoani Mwanza, Revocatus Mkama amejishindia fedha hizo, wanaoshuhudia kushoto ni Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, kulia ni Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom, Bi. Reenu Verma.
Mtaalamu wa Mawasiliano ya Teknologia wa Vodacom Tanzania Tulisindo Rashid kushoto, akifuatilia jinsi komputa inavyochezesha nambari za washiriki wa droo kubwa ya mwezi ya kumpata mshindi wa Mlioni 10 wa promosheni ya M-PESA, ambapo Mkazi wa Kitangiri Mkoani Mwanza, Revocatus Mkama amejishindia fedha hizo, wanaoshuhudia wa pili toka kushoto ni Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, Meneja Mawahusiano Matina Nkurlu, Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom, Bi. Reenu Verma.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII