SIMBA KAZINI LEO!
By Maganga Media - May 13, 2012
SIMBA leo itakuwa uwanjani Sudan kumenyana na Al Ahly Shendi ya huko katika mechi ya pili ya raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho. Simba iliondoka jijini Jumanne kuelekea Sudan kwa ajili ya mechi hiyo ambapo hata hivyo hawakupata mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji wao hali ilioufanya uongozi wa klabu hiyo kuazimia kupeleka malalamiko (CAF).
Simba leo inahitaji ushindi au kama kufungwa isiwe zaidi ya mabao 3-0 ili isonge mbele hatua inayofuata ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga Simba imefanyiwa vitendo ambavyo si vya kiuanamichezo ikiwa ni pamoja na kusafirishwa umbali mrefu, kupewa chakula usiku sana pamoja na kulazwa kwenye hosteli badala ya hoteli nzuri kama walivyofanyiwa wao
walipofika nchini.
“Kila kitu chetu kwa upande wa benchi la ufundi kiko sawa, pamoja na vurugu zao lakini tunaamini dakika 90 uwanjani ndio zitaongea,” alisema Kamwaga.
“Wachezaji wako kwenye ari kubwa pamoja na mizengwe ya hapa na pale, kwani hawakukatishwa tamaa badala yake walifanya mazoezi wenyewe pamoja na kocha kuwapa
mapumziko… wachezaji wanasema lengo lao ni kuvuka raundi inayofuata na watavuka hata wakiwafanyiwa vituko,”alisema Kamwaga.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII