Manchester City yakaribia ubingwa!
By Maganga Media - May 7, 2012
Manchester City imesogea karibu kabisa ya mfundo wa kumalizia Ligi Kuu ya Engald na kutangazwa mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 44, baada ya Yaya Toure kufunga mabao mawili na kuipatia ushindi wa mabao 2-0 timu yake dhidi ya Newcastle United.
Kiungo huyo anayechezea pia timu ya taifa ya The Ivory Coast alifanikiwa kumfunga mlinda mlango Tim Krull kwa mkwaju maridadi wa kimo cha beberu zikiwa zimesalia dakika 20 kabla mpira kumalizika.
Manchester City sasa wanafahamu fika iwapo watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya QPR katika mechi ya kumalizia msimu, basi watatangazwa moja kwa moja mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya kandanda ya England.
Ulikuwa uwanja huo huo wa Newcastle tarehe 11 mwezi wa Mei mwaka 1968 ambapo Manchester City walinyakua ubingwa wa ligi kwa mara ya mwisho. Takriban miaka 44 baadae inaonekana historia ipo njiani kujirudia huku klabu hiyo ikisogea mbele ya Manchester United ambao waliokuwa wanaongoza ligi hiyo kwa muda mrefu.
Meneja wa United, Alex Ferguson. Wanahitaji miujiza kutetea unigwa wao |
Manchester United wameendelea kuweka ndoto zao za kutetea ubingwa wao kwa kuichapa Swansea kwa mabao 2-0. United walijitahidi kutaka kufunga mabao mengi ili kupunguza tofauti iliyopo kati yao na Manchester City, lakini walipoteza nafasi nyingi za kufanikisha hilo. Paul Scholes ndio aliandika bao la kwanza la United huku la pili likifungwa na Ashley Young.
Manchester City watatangazwa kuwa mabingwa wiki ijayo iwapo wataichapa QPR, hata kama Manchester United watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Sunderland.
Iwapo United watataka kuchukua ubingwa, watalazimika kupata ushindi wa magoli zaidi ya manane huku wakizingatia matokeo yatakayopatikana kati ya City na QPR.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII