HABARI MPYA LEO  

Wapinga ongezeko la nauli TRL

By Maganga Media - May 11, 2012

WADAU wa Usafiri Nchini, wamepinga maombi ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutaka kuwe na kuongeza nauli kwa abiria wanaotumia usafiri wa treni na kuitaka Serikali, kuingilia kati kwa kuchukua jukumu la kusimamia huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.

Wadai hao waifanya hivyo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kukusanya maoni juu ya mapendekezo ya kutaka kuwepo kwa ongezeko la nauli kwa abiria wanaotumia usafiri wa treni.

Wakizungumza katika mkutano huo, wadau walisema kwa sasa TRL, isifikirie kuongeza nauli kwa abiria kwa sababu huduma inazozitoa za kiwango cha chini na kwamba kinachotakiwa sasa ni kwa kampuni hiyo kujipanga ili baadaye iweze kutoa huduma bora.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Walaji wa Huduma zinazodhibitiwa na Sumatra (Sumatra CCC), Oscar Kikoyo, alisema Baraza halikubaliani na ombi la TRL,  a kutaka kuongeza nauli kwa zaidi ya asilimia 50.

Alisenma ombi hilo halilengi katika kuwatendea haki watumiaji wa usafiri huo.

Alisema watumiaji wengi wa huduma za TRL, ni watu wa vipato vya chini na kwamba ongezeko la naui kwa iwango cha kati ya asilimia 50 hadi 52 litawaumiza.

“Takwimu zinaonyesha kwamba mchango wa nauli katika pato la TRL, ni asilimia 14 za  gharama za uendeshaji ambapo mwaka 2009, nauli za abiria zilichangia asilimia 17.8 na kwenye pato la jumla mwaka 2010 TRL, iichangia asilimia 14.3,”alisema.

Kakoyo alibainisha kuwa TRL, ni mali ya Serikali  kwa asilimia 100 na kwamba sasa wakati umefika kwa Serikali kuwekeza mtaji mkubwa ili  kuboresha huduma za TRL.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII