HABARI MPYA LEO  

JAMANI MAZINGIRA YETU!

By Maganga Media - May 7, 2012

Wito umetolewa kwa wanachuo wa Chuo kikuu cha Dodoma kutunza mazingira yetu kwani kila mtu anaelewa umuhimu wa mazingira. Kwa mujibu wa chanza cha habari hii mtu yeyote atakayekamatwa anakatisha sehemu isiyo stahili atakabiliwa na adhabu kali. Chonde chonde tuyanusuru mazingira yetu kwa kizazi cha sasa na cha baadae.
Kafteria ya Humanities ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika sana na suala la watu kukatisha bila kuzingatia njia zilizotengenezwa na mchina kama wenyewe mnavyopenda kuziita
Njia kuu ya kutoka darasani kuelekea Hosteli Skuli ya SH
Wengine nao haoooooooooo wanajiachia kwenye njia zisizo sahihi. Kazi ipo ila ni vizuri kama msomi ukajiongeza tu. Tupo Dodoma sehemu yenye ukame ila kama mazingira yakitunzwa vizuri mwenyewe utapakubali
SI BUSARA HATA KIDOGO KUELEKEZWA NJIA KWA KUWEKEWA MIBA KAMA UNAZUIA MBUZI AU KUKU KWENYE BUSTANI YA MBOGA MBOGA. TUNZA MAZINGIRA!
 Pamoja na kuweka miba kuonesha kuwa sehemu hairuhusiwi kupita jamaa anaonekana kutojali kabisa.
 Tuunge mkono jitihada za kutunza mazingira yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.
Hii sio njia sahihi.
Habari zilizothibitishwa zimesema kuwa kuanzia sasa atakayepita sehemu isiyoruhusiwa adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwani ni kinyume na by laws za ukaaji wa Hosteli. Chukua tahadhari!

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII