Diwani Wa CCM Afikishwa Mahakamani kwa Kutishia Kumuua Mbunge Na Diwani Wa Chadema
By Maganga Media - May 16, 2012
Mbunge wa Iringa(Chadema) Akiongea na wafuasi wa chadema baada ya kesi kuhairishwa mpaka tarehe 30/5/2012 itakapotajwa tena |
Wananchi Wakisubiri Kusikiliza Kesi Mahakamani Mapema leo |
Mtuhumiwa Wa kutishia Mauaji Diwani wa CCM kata ya Nduli Idd Chonanga akiwasili mahakamani tayari kwa kusomewa mashitaka yanayomkabili |
Mbunge wa iringa Mjini Mch Peter Msigwa(Chadema) akifuatilia Kesi ndani chumba cha mahakama ya mkoa Iringa |
Kutoka mahakamani
Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Bi Consolata Singano akiendesha kesi huku akiongozwa na msoma mashtaka wa serikali Ndg msuya, alisema kuwa Mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa mawili, moja likiwa ni mnamo tarehe 14/5/2012 katika ofisi za manispaa ya Iringa alimtishia kwa maneno Kumuua Mbunge wa Iringa mjini mch Peter Msigwa, shitaka la Pili, tarehe hiyo hiyo alimtishia kumuua diwani wa kata ya Mivinjeni(Chadema) Ndg Fredrick Nyalusi. Mshitakiwa alikana mashtaka, hakimu alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa, lakini wadhamini wa mshtakiwa hawakutimiza masharti ya dhamana hivyo amepelekwa rumande.
Mbunge Msigwa naye asema haya

Mbunge wa iringa Mch Peter msigwa amewataka wananchi wa iringa kuwa watulivu katika kipindi cha vurugu za kisiasa, wasiwe chanzo cha fujo na machafuko ya aina yoyote na waendelee na shughuli za ujenzi wa taifa kama kawaida, ingawa ameshangaa mpaka sasa hakuna kiongozi wa serikari ya mkoa aliyekemea kitendo hicho kisichokuwa cha kiungwana.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII