HABARI MPYA LEO  

Diamond awafagilia Wacheza shoo

By Maganga Media - May 6, 2012





MSANII anayeogopwa na wasanii kwa kuwa mkali wa jukwaani, Diamond Plutnumz amesema kuwa anawaamini na kuwaheshimu wacheza shoo wake kwani ndio wanaompa sapoti kubwa katika kazi zake.

"Unajua kikubwa hasa ninachokifanya ni kushirikiana na watu na siku zote siwezi kufanya kazi peke yake pasipo kuwa na wacheza shoo wangu kwani ndio wanaonipa sapoti kubwa na kubadilishana mawazo ili kuleta vionjo vipya.

"Mimi sina ubahili hasa ninapofanya kazi, na hili ndilo lililonifanya nizidi kusonga mbele katika kazi ya muziki ili upate ni lazima utoe, ili nifurahishe mashabiki ni lazima nizingatie kanuni kama hizi" anasema.

Diamond anaongeza kwamba maandalizi ni silaha nyingine ambayo inamfanya kila siku mashabiki wamwone mpya "siwezi kutokeza machoni mwa mashabiki nikiwa vivyo hivyo kila siku hata nikiwa na wimbo mpya sidhani kama watanifurahia kila siku staili hizohizo, pia namtanguliza Mungu katika kila jambo" anasema.

Hata hivyo amewashukuru mashabiki na kuahidi kutowaangusha "nawashkuru sana na nawaahidi kuwa sitowaangusha na wategemee vitu vipya".

Wikiendi iliyopita msanii huyu alifanya shoo katika sehemu ya kiburudani ya Dar Live iliyopo jijini Dar es Salaam na kuvunja rekodi kwa kuingiza mashabiki wengi zaidi kuliko shoo zote zilizowahi kufanyika sehemu hiyo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII