HABARI MPYA LEO  

Wazee China wafika Milioni 120

By Maganga Media - Apr 9, 2012

Serikali ya China imeeleza kutoa kipaumbele suala la afya ya wazee katika juhudi za kukabliana na changamoto ya idadi kubwa ya wazee. Kauli hiyo imetolewa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya afya duniani, ambayo ni leo tarehe 7 Aprili. 

Shirika la afya duniani limeamua kauli mbiu ya siku ya afya kwa mwaka huu ni "jamii yenye idadi kubwa ya wazee na suala la afya". 

Hivi sasa, idadi ya wazee wenye umri wa miaka 65 na zaidi nchini China imefikia milioni 120, ambayo ni sawa na asilimia 9 ya watu wote nchini China. Serikali ya China imeahidi kuinua kiwango cha afya kwa wazee na kuhakikisha wazee wanapata huduma za matibabu. Kwa mujibu wa mpango wa serikali, kabla ya mwaka 2015 China inalenga kuongeza vitanda zaidi ya milioni 3.4 katika makazi mbalimbali yanayowahudumia wazee, pia zahanati kote nchini zinatakiwa kutoa huduma za matibabu kwa wazee na kufuatilia hali ya afya ya wazee wenye umri wa miaka 65 na zaidi. 

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya wanawake nchini China ilikuwa milioni 620, ikichukua asilimia 48.5 ya idadi yote ya watu nchini China. Serikali ya China inatilia maanani sana maendeleo ya wanawake, kuifanya sera ya usawa kati ya wanaume na wanawake kama sera mojawapo ya kimsingi ya kitaifa katika kusukuma mbele maendeleo ya jamii. Wakati inapotunga sera za jumla, serikali ya China hufuata kanuni za kuwashirikisha kwa usawa wanaume na wanawake na kuhimiza maendeleo ya pamoja. Serikali ya China imetoa uhakikisho imara wa kisiasa na dhamana ya kisheria kwa maendeleo ya wanawake.

Kuanzia katikati ya miaka ya tisini ya karne iliyopita, serikali ya China imetoa "Mwongozo wa Maendeleo ya wanawake wa China" wa miaka mitano na miaka kumi, ambao umelinda kihalisi haki na maslahi halali ya wanawake, kuboresha mazingira ya kijamii ya maendeleo ya wanawake nchini China na kusukuma mbele maendeleo ya pande zote ya kazi ya wanawake. Wanawake wa China si kama tu wana haki sawa na wanaume katika maeneo ya siasa, uchumi, jamii, utamaduni na nyumbani, na haki zao maalum zinafuatiliwa zaidi na serikali na jamii. Chini ya juhudi za pamoja, hadhi ya wanawake nchini China imeinuka kidhahiri, hali ya wanawake imeboreshwa na maendeleo ya wanawake nchini China yameingia katika kipindi kizuri.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII