HABARI MPYA LEO  

Kiduku champigisha faini Mnyika

By Maganga Media - Apr 9, 2012



MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, juzi alijigomboa kwa gharama ya sh 20,000, ili asicheze kiduku katika sherehe za kutimiza miaka 60 ya mmoja wa wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika jimbo hilo.

Katika sherehe hizo zilizofanyika ukumbi wa Shaku Manzese; mzee aliyekuwa akifanya sherehe yake ya kuzaliwa ni Hamad Ukwesule, ambapo Mnyika alialikwa kuwa mgeni rasmi.
Mshereheshaji wa shughuli hiyo, Boniface Jacob, ambaye ni Diwani wa Ubungo, alitumia utaratibu wa kumuita mtu mmoja mmoja kwenda mbele kwa ajili ya kuonesha burudani na anayefanikiwa, anamtaja mtu mwingine kwa ajili ya kuendeleza burudani hiyo ukumbini huku wale wanaoshindwa wakilazimika kulipa faini.

Akizungumza mara baada ya kulipa faini, Mnyika alisema hakuwa amejiandaa kwa ajili ya kucheza na kwamba hali hiyo ilikuwa ya kumshtukiza pale ukumbini. “Mimi wangeniambia kama kuna nafasi ya kucheza ukumbini, mbona ningejiandaa tu….isipokuwa nilijua hapa ni sehemu ya kubadilishana mawazo pasipo kucheza,” alisema Mnyika huku akicheka.

Alielezea kuwa sherehe za namna hiyo zinapaswa kuendelezwa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kuwafikisha wazee wa aina hiyo katika umri huo, huku wakiuona ukweli wa mabadiliko ya nchi, kiuchumi na maendeleo ambayo CHADEMA inayapigania

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII