Mutharika Mahututi, apelekwa Afrika Kusini
By Maganga Media - Apr 6, 2012
Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika |
Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika aliyekuwa amelazwa hospitalini baada ya kupatwa na mshutuko wa moyo amesafirishwa kwenda Johannesburg kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuzidiwa zaidi na kulazwa akiwa mahututi katika hopsitali moja mjini Lilongwe baada ya kuanguka asubuhi.
Mkewe Callista Mutharika pamoja na kakake Peter Mutharika walimtembelea kiongozi huyo hospitalini.Japo haijathibitishwa rasmi ikiwa hali ya afya ya rais huyo inamuzuia kuongoza nchi, katiba ya taifa inampa uwezo Makamu wa Rais kuongoza endapo rais ameondoka madarakani kwa namna moja au nyingine.
Kabla ya tamko hilo Bi Banda vyombo vyote vya habari vilikuwa vimebana kutoa habari zozote kuhus hali ya raia Bingu wa Mutharika. Lakini baada ya Makamu wa rais kufichua kuwa Kiongozi wao ni mgonjwa, ndipo Radio ya kitaifa ikatangaza kuwa Mutharika atapelekwa Afrika kusini kwa matibabu maalum.
Kulingana na katiba ya Malawi ikiwa Mutharika atashindwa kuendelea na kazi yake ya Urais basi Makamu wake Bi Joyce Banda atalazimika kushikilia hatamu za uongozi kwa kipindi kilichosalia . Hata hivyo Bi banda na rais Mutharika walikuwa hawasikilizani kwani walikosana mwaka wa 2009 na Makamu huyo wa Rais akalazimika kuhamia upinzani.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII