JOKATE NA DIAMOND WAZUA BALAA JINGINE
By Maganga Media - Apr 6, 2012
ACHANA na kitendo cha Naseeb Abdul ‘Diamond’ kukataa kupokea fedha alizotuzwa na zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu katika shoo ya Diamond are Forever ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Ijumaa iliyopita, kuna vitu vingine viliwaacha wadau na maswali kibao katika shoo hiyo
Wadau waliofurika ukumbi humo walikuwa wakifuatilia vitendo walivyokuwa wakifanya Diamond na mlimbwende namba mbili wa Tanzania mwaka 2006, Jokate Mwegelo hatua kwa hatua.
Diamond na Jokate waliingia ukumbini pamoja wakiwa ndani ya gari aina ya Benz lenye rangi ya darkblue huku wakiwa na mama mzazi wa staa huyo.
Mbali na Jokate, Diamond na mama yake, pia ndani ya gari hilo alikuwepo msichana mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Wa kwanza kushuka alikuwa ni Diamond akafuatia mama yake, baadaye akashuka msichana asiyetambuliwa na mwisho akashuka Jokate.
Kitu kingine kilichowaacha wadau midomo wazi ni kitendo cha mama Diamond kupiga picha na Jokate wakati walipokuwa wakipita kwenye zulia jekundu. Wawili hao walisimama na kuweka pozi, kisha kufotolewa picha kadhaa.
Kitendo hicho cha kupiga picha na mama Diamond siku za nyuma kilikuwa kikifanywa na Wema wakati alipokuwa mchumba wa staa huyo anayevuma na kibao cha Nimpende Nani.
Kabla ya tukio hilo, Jokate alikuwa akikwepa kupiga picha hiyo pamoja na kuombwa kufanya hivyo, hata hivyo jitihada za mama Diamond zilisaidia baada ya kumsihi ‘mwanaye’ huyo waweke kumbukumbu ya picha.
“Mwanangu sogea basi wenzio wapige picha,” alisema mama Diamond huku Diamond akiwa amesimama pembeni akishuhudia zoezi hilo katika hali ya kumbembeleza Jokate.
Tukio lingine lililozua minong’ono ni lile la Diamond kutuzwa ‘t-shirt’ iliyokuwa na picha ya msichana mwenye kidoti usoni, awali baada ya kuipokea Diamond alitishia kuelekea kwenye meza aliyokuwa amekaa Wema lakini baadaye akabadili mwelekeo na kwenda kumpa fulana hiyo Jokate.

“Kuna nini pale, kwa nini Diamond asiende kumpa mama yake fulana ile?” alihoji mdau mmoja aliyekuwa akifuatilia mambo ndani ya ukumbi huo.
Kama vile haitoshi, mara kadhaa Diamond alikuwa akishuka jukwaani na kwenda katika meza aliyokuwa amekaa Jokate na wenzake na kuanza kucheza kwa staili ya kuzungusha nyonga pamoja nao.
Shoo ilipoisha baada ya umeme kuleta hitilafu, hakuna aliyejua Jokate na Diamond kama waliondoka pamoja kutoka ukumbini au vinginevyo.
Hata hivyo, kuna madai kuwa, Jokate alitangulia nyuma ya jukwaa na Diamond alipomaliza kukusanya baadhi ya vitu vyake akamfuata huko na kisha kuishia zao.
Siku za nyuma kulikuwa na madai kwamba wawili hao ni wapenzi, baada ya Wema kudai kuwa amemfumania Diamond na Jokate lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha madai hayo.

MPEKUZI
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII